Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

NCHI wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) zimeshauriwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika jumuiya hiyo kunufaisha wananchi walio ndani ya jumuiya na hiyo ni pamoja na uwekaji wazi wa mikataba ambayo serikali inaingia na makampuni mbalimbali hasa katika sekta za madini, mafuta na gesi asilia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa taasisi ya kimataifa ya uhamasishaji na uwajibikaji wa mapato yatokanayo na sekta ya uziduaji (mafuta, gesi asilia na madini) Ludovick.

Utouh amesema kuwa tukio la leo ni mwendelezo wa mikutano wa SADC inayoendelea nchini kabla ya kuhitimishwa kwa mkutano wa wakuu wa nchi na serikali utakaofanyika Agosti 17 na 18 na mazungumzo hayo yamezungumzia juunya uwekaji wazi wa mikataba ambayo serikali inaingia na wawekezaji katika rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia rasilimali ambazo nyingi hugunduliwa na wananchi lakini hawashirikishwi katika masuala hayo hali inayopelekea hata kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Amesema kupitia taasisi kimataifa ya uhamasishaji na uwajibikaji wa mapato yanayotokana na sekta ya uziduaji yenye makao makuu nchini Norway na yeye akiwa mwenyekiti wamedhamiria kuwa hadi kufikia mwaka 2021 nchi zote wanachama wa SADC ziwe na utaratibu wa kuweka mikataba wazi ambapo hadi sasa nchi nane wanachama ikiwemo Tanzania wamekwisha weka mikataba yao wazi ili wananchi waweze kujiridhisha na kile ambacho kinafanywa juu ya rasilimali hizo.

Aidha amesema kuwa nchi nane ambazo ni wanachama ikiwemo Tanzania tayari zimeweka mikataba ya sekta ya uziduaji hadharani na nchi mbili ambazo sio wanachama wa taasisi hiyo ya kimataifa wameweka wazi mikataba yao na nchi sita ambazo ni wanachama wa SADC bado hazijaweka wazi mikataba yao ambayo kwa ujumla ambayo husaidia kupunguza rushwa na kuweka uwazi kwa wananchi, serikali na wawekezaji Kama ikiwekwa wazi.

Pia Utouh ameeleza kuwa nchi za Afrika Zina rasilimali za kutosha ambazo haziwezi kudumu milele hivyo ni vyema mapato yatokanayo na rasilimali hizo yakaelekezwa kwenye maendeleo ya kizazi cha Sasa na baadaye.

Kwa upande wake mratibu wa shirika la Zimbabwe Environment Legal Association Nyaradzo Mutonhori amesema kuwa ni haki ya kila mwananchi kujua uwazi wa mikataba inayoingiwa na wawekezaji;

" Tuna haki ya kujua kwa uwazi kabisa juu ya mikataba hiyo, kwa kuwa tunawaona wawekezaji hivyo tungependa kujua wanachochukua na wananchi wanavyonufaika, pia kuweka wazi mikataba hiyo Kuna faida kwa wananchi kuibariki." ameeleza Nyaradzo.

Nyaradzo amesema kuwa nchi wanachama wa SADC waangalie namna ya kuondoa usiri baina ya serikali na kampuni mbalimbali za uwekezaji pamoja na kubainisha muda mahususi ambao kampuni za uwekezaji umewekeza katika rasilimali husika.

Kwa upande wake mratibu wa mtandao wa haki rasilimali nchini Rachel Chagonja amesema kuwa rasilimali zinazopatikana katika nchi jumuiya za SADC ni vyema zikatumika kunufaisha nchi wanachama wa jumuiya hiyo na sio kufuja rasilimali hizo bila kuangalia kizazi kijacho kitanufaika vipi, hivyo suala la uwazi wa mikataba lazima lizingatiwe ili keki ya taifa igawanywe kwa usawa.

Rachel ameeleza kuwa rasilimali sio za watu wachache na serikali ndio madalali wa wananchi hivyo mrejesho wa namna rasilimali hizo zinavyotumika ni muhimu kuwa wazi pamoja kueleza namna mapato ya rasilimali hizo yanavyochangia katika sekta za maendeleo.
Wawasilishaji wa mada mbalimbali wakiwa katika picha pamoja, leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa taasisi ya kimataifa ya uhamasishaji na uwajibikaji wa mapato yanayotokana na sekta ya uziduaji (mafuta, madini na gesi asilia) Ludovick Utouh akizungumza katika mkutano huo ambapo ameeleza kuwa kuwekwa wazi kwa mikataba kunasaidia katika kupunguza rushwa pamoja na kuweka uwazi kwa wananchi, serikali na wawekezaji leo jijini Dar es Salaam.
Mtoa mada kutoka nchini Botswana Robert Letsatsi akichangia mada katika mkutano huo ambapo ameeleza kuwa nchi jumuiya lazima ziangalia kwa jicho la tatu masuala ya rushwa, uwazi na usawa ili kuweza kufika mbali zaidi leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shirika la Zimbabwe Environment Legal Association (ZELA) Nyaradzo Mitonhori akizungumza katika mkutano huo na kueleza kuwa nchi jumuiya ya SADC ziangalie namna ya kuondoa usiri baina ya serikali na kampuni za uwekezaji leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Zimbabwe, Botswana na Msumbiji wakifuatilia mkutano huo, ambapo kwa kiasi kikubwa suala la uwazi wa mikataba baina ya serikali na kampuni za uwekezaji limejadiliwa, leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mtandao wa haki rasilimali nchini Rachel Chagonja akizungumza katika mkutano huo ambapo ameeleza kuwa serikali ndio dalali kwa wananchi wake hivyo lazima waangalie suala la uwazi ili kila mwananchi anufaike na rasilimali hizo leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...