Na Khadija seif, Michuzi tv
CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke.

Akizungumza na waandishi wahabari Mwenyekiti wa chama hicho Fred sumari (Dile) amesema Ni wakati wa serikali kutambua kuwa kuna vipaji vingi vinazalishwa katika wilaya hiyo .

"Mzee jongo,Rashid Matumla,Joketi Mwegelo,Tmk wanaume,yamoto band pamoja na Mchezaji mpira anaefanya vizuri nchi za nje Mbwana samata wote Ni zao la wilaya ya Temeke,"

Aidha, Sumari ameeleza bila kificho Temeke ndio sehemu peke inayoleta chimbuko la watu maarufu na kuthibitisha Hilo wameamua kuandaa tamasha kubwa la waigizaji wa wilaya ya Temeke lengo ni kuwakutanisha wasanii wote wa wilaya hiyo pamoja na kujenga umoja,mshikamano na nguvu ili kuwapa ushirikiano wasanii chipukizi wenye vipaji.
Kwa upande wake Msanii wa Maigizo Madebe lidai amesema hata serikali inawasahau sana wasanii wa Temeke hasa likija swala la fursa .

"Kwa umoja wetu tumekusanyana na kuandaa tamasha kubwa la kazi za Sanaa linalotarajiwa kufanyika Agosti 25 mwaka huu katika ukumbi wa  harbours club uliopo mivinjeni kurasini,"

Sanajari na hilo lidai ameeleza kuwa kutapambwa na burudani mbalimbali kama kucheza Rede,kukuna Nazi kwa wakina Baba,kuimba,vichekesho pamoja na  filamu fupi itakayochezwa na wasanii elfu 1000 huku  muimbaji mkongwe wa Taarab Patricia Hillary kuupamba usiku huo.

Pia amesema lengo lingine la tamasha  hilo ni kukuza na kunyanyua soko la filamu kwa wasanii na wazalishaji kwa upande wa Temeke.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...