Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MSIMU wa tatu wa Mashindano ya Sprite Bball Kings hatua ya mtoano imefanyika leo kwa timu 43 kushuka dimbani kutafuta tu 15 zitakazocheza kwenye hatua ya 16 bora.

Mechi hizo zilizoanza majira ya saa 2 asubuhi kwenye Viwanja vya JMK Park zilikuwa na ushindani mkubwa sana huku timu ngeni zikionekana kujiandaa vizuri.

Msemaji wa mashindano hayo Goza Chuma amesema kwa mwaka huu ushindani umekuwa ni mkubwa sana, timu zimejiandaa kuja kusaka kitita Milioni 10 zitakazoshindaniwa kwa mshindi wa kwanza.

Goza amesema, msimu huu wa tatu wa Sprite Bball Kings umeleta fursa kwa vijana kwani mchezo wa kikapu ni ajira tofauti na mawazo ya zamani ya watu kuwa unachezwa na vijana waliosoma au mabishoo.

“Mwaka huu watu wanaweza kuona idadi ya timu zimepungua ila sio kama mashindano yamekosa ubora hapana ila msimu huu watu wamejipanga sana na unapoona hapa hakuna timu iliyopota kwa walk over kwani zote zimefika tofauti na misimu iliyopota,” amesema Goza.
“Sheria za mwaka huu zimebadilika, misimu miwili tuliweka sheria ya kuwa na wachezaji watatu wa ligi kuu ila kwa msimu huu ni wachezaji sita kwahiyo nyie wenyewe mtaona ni ushindani wa aina gani utakaokuwepo kwenye msimu wa mwaka huu,”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...