Mmoja wa wafugaji wa ng'ombe wa nyama Tajiri Kalanga akipokea cheki kutoka kwa Naibu waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega,Kushoto kwake ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Ghambo,kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Mbulu na Mbulu,
Baadhi ya mshiriki wa maonyesho ya nanenane upande wa wafugaji akipokea kombe kutoka kwa mgeni rasmi Naibu waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega.
Naibu waziri wa Mifugo ,Kilimo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega akizungumza katika viwanja vya maonyesho ya nanenane Themi Mkoani Arusha.
Baadhi ya washiriki na wananchi waliojitokeza katika maonyesho ya sherehe za nanenane leo kanda ya kaskazini katika viwanja vya Themi Njiro mkoani Arusha.
Baadhi ya washiriki na wananchi waliojitokeza katika maonyesho ya sherehe za nanenane leo kanda ya kaskazini katika viwanja vya Themi Njiro mkoani Arusha.
Baadhi ya washiriki na wananchi waliojitokeza katika maonyesho ya sherehe za nanenane leo kanda ya kaskazini katika viwanja vya Themi Njiro mkoani Arusha.Picha zote na Vero Ignatus
Mfugaji ndugu Tajiri Kalanga akiwa mbele ya mgeni rasmi mara baada ya kuibuka kuwa mshindi wa Pili katika paredi ya mifugo ng'ombe wa nyama.kushoto kwake mkuu wa mkoa wa Arusha,kulia kwake mkuu wa mkoa wa Arusha


Na.Vero Ignatus,Arusha


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amefunga rasmi maonesho ya Kilimo na Mifugo Kanda ya Kaskazini katika viwanja vya Taso Themi Jijini Arusha.

Akizungumza mara baada ya kutembelea maonesho hayo Ulega amesema kuwa amefurahishwa na Paredi ya Mifugo aliyoiona Uwanjani hapo na kuupongeza mkoa wa Arusha kwa kuwa wafugaji wamekuwa na mifugo bora tofauti na alivyodhani.

Amesema katika maonesho hayo amezoea kuona mifugo bora inatoka kwa Taasisi za Serikalini kama Ranchi ya Taifa (NARCO),Jeshi la Magereza lakini wafugaji kutoka wilaya za Monduli,Longido,Ngorongoro ndio wameibuka Vinara kwa Mifugo bora.

Hata hivyo amezitaka Taasisi mbali mbali viwanjani hapo kutoa taarifa za vipeperushi kwa wakulima na wafugaji tofauti na maelezo ili kuwawezesha,wakulima na wafugaji kutunza kumbukumbu kwa hapo baadae kwa kuwa hawawezi kukumbuka kila kitu.

Ulega amesema amefurahishwa na Tasisi za fedha ambazo zimeonesha kuwasaidia wakulima na wafugaji viwanjani hapo kuwapa mitaji kwa kuwa ni changamoto ambayo imekuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu sasa.

Amesema Serikali itafurahishwa endapo itaona uwekezaji mkubwa wa viwanda vya kusindika mazao ya Kilimo na kuchakata Mifugo,kwa kuwa mikoa ya Kilimanjaro ,manyara na Arusha uwepo wa rasilimali ni mkubwa.

Maonesho hayo yamefungwa rasmi leo lakini yataendelea hadi siku ya Jumatatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...