*Asema watazidi kushiriki katika kuimarisha sekta za afya, maji, elimu na kuwainua kiuchumi wanawake, vijana na walemavu

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

BALOZI wa China nchini Wang Ke amesema kuwa ushirikiano wa baina ya China na Tanzania unazidi kuimarika na mwaka huu mahusiano hayo yanatimiza miaka 55 na kueleza kuwa wao kama viongozi wataendelea kuhakikisha mahusiano hayo yanazidi kuimarika na hiyo ni pamoja na kushirikiana katika shughuli za kiuchumi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa tuzo na zawadi kwa washindi wa uandishi wa insha za kudumisha mahusiano baina ya Tanzania na China ambapo wanafunzi wa vyuo mbalimbali walishiriki, Balozi wa China nchini Wang Ke ameeleza kuwa mashindano hayo yalilenga kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na China na washindi wa shindano waliandika insha za kusisimua kuhusiana na mahusiano ya nchi za Tanzania na China.

"Tutaendelea kuyapeleka mahusiano yetu mbali zaidi, na tutaendelea kushiriki katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo elimu, afya, na maji pamoja na kuwasaidia vijana katika shughuli za kimaendeleo ili kujenga kizazi bora" ameeleza Wang Ke.

Balozi Wang amesema kuwa zaidi ya watalii 3000 kutoka China Tanzania na mwaka huu wanategemea kuzindua rasmi safari za ndege kupitia shirika la ndege nchini (Air Tanzania) kutoka Guangzhou, China na Dar es Salaam hali inayotegemewa kuongeza ushirikiano zaidi.

Kwa upande wake mshindi wa kwanza wa mashindano hayo Humphrey Mrema amesema kuwa mahusiano ya nchi hizo mbili yana tija na viongozi wao wanaonesha jitihada za kuwaandaa vijana watakaoendeleza mahusiano hayo.

Mrema ameishukuru serikali ya China naTanzania na kusema kuwa atawasilisha andiko lake linalohusu upatikanaji wa taulo za kike kwa ubalozi wa China ili kuwazesha kuwasadia wasichana wa shule hasa wa vijijini ambao wanakosa taulo hizo na kuathiri masomo yao.
Washindi wa uandishi wa insha wakiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Wang Ke pamoja na viongozi mbalimbali,leo jijini Dar es Salaam.

 .Balozi wa China  nchini Wang ke akizungumza mara baada ya kukabidhi tuzo hizo ambapo amesema kuwa mahusiano hayo yataendelea kudumu na yataenda sambamba na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kiuchumi, Leo jijini Dar es Salaam.
 Mshindi wa kwanza wa mashindano hayo Humphrey Mrema (kulia) akimkabidhi zawadi ya chupa iliyonakshiwa bendera za Tanzania na China balozi wa China nchini Wang Ke Kama ishara ya shukrani, leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi wa washiriki waliojitokeza kushuhudia utoaji wa tuzo hizo za uandishi insha za kudumisha mahusiano baina ya China na Tanzania, leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...