*Rais Magufuli asifiwa kwa utendaji kazi, aungwa mkono, SADC kuleta mabadiliko chanya kwa wenye viwanda
*Kiwanda cha Keda Ceremics Limited kulipa kodi ya zaidi ya dola milioni 12 kwa Serikali
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WIKI
ya nne ya viwanda imehitimishwa kwa washiriki wa maonesho hayo kutoa
nchi mbalimbali ndani ya jumuiya ya SADC kutembelea viwanda mbalimbali
Tanzania bara na visiwani na kujionea namna viwanda hivyo vinavyofanya
kazi pamoja na kutengeneza fursa mbalimbali hasa za masoko kwa
wanajumuiya hao.
Ziara
iliyofanywa katika kiwanda cha usindikaji wa matunda cha Elven agri
kilichopo Mapinga Bagamoyo Mkoani Pwani walishiriki walijionea namna
matunda yanavyochakatwa na kukaushwa na baadaye kusafirishwa katika nchi
mbalimbali ndani ya jumuiya ikiwemo Botswana na Zambia pamoja na nchi
za nje ikiwemo Marekani, kiwanda hicho chenye takribani ya heka 900
kinatoa ajira kwa wanawake na vijana pamoja na kushiriki shughuli za
kiuchumi na kijamii ikiwemo kujenga shule pamoja na miundombinu ya maji.
Msimamizi
wa kiwanda hicho Martin Matembo amesema kuwa bidhaa za matunda yakiwemo
maembe, nanasi, papai, na ndizi zinazosindikwa kiwandani hapo zinauzwa
nchini pamoja na kupelekwa nje ya nchi na kupitia SADC wamepata fursa
kubwa kupitia wiki ya viwanda kwani wamejenga mahusiano bora na
makubaliano ya kibiashara na washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za
Afrika Kusini, Zambia na Botswana.
Amesema
kuwa mkutano mkuu wa 39 wa wakuu wa nchi na serikali utaleta mabadiliko
chanya nchini hasa kwa wenye viwanda katika jumuiya hiyo, na
amesisitiza ushirikiano ndani ya jumuiya hiyo ili kuleta ushindani
katika soko la dunia.
Kiwanda
cha pili kilichotembelewa ni cha Motisun Group kilichopo Chalinze
Mkoani Pwani ambacho kina viwanda vinavyozalisha bidhaa za plastiki,
vinywaji, mabati pamoja na rangi za nyumba (kiboko paints).
Kiwanda
hicho kinachozaliwa sharubati (juisi) ni matokeo ya jitihada za Rais
Dkt. John Magufuli katika kujenga nchi ya viwanda na kupitia kiwanda
hicho wakulima wamekuwa wanafaidika kwa kuwa kiwanda hununua matunda
kutoka kwa mkulima yeyote huku uhitaji wa matunda kwa kiwanda hicho
ukifika tani 300 kwa siku.
Abubakar
Mlawa mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano wa kiwanda hicho ameeleza kuwa
kupitia maonesho hayo ya viwanda lazima wananchi wajifunze kupenda na
kuthamini bidhaa za ndani;
"Mahitaji
ya juisi ni makubwa sana hasa katika nchi za Zambia, Kongo na Malawi
ila tuna changamoto ya maji, tunahitaji maji zaidi ya lita milioni mbili
kwa siku kwa ajili ya uendeshaji lakini tunapata maji lita laki tano hivyo
tunaomba Serikali itusaidie tuweze kupata maji kutoka mto Ruvu" ameeleza
Mlawa.
Kiwanda
hicho ambacho hulipa kodi kwa serikali takribani zaidi ya shilingi
milioni 700 kimetoa ajira kwa wazawa kwa asilimia 95, huku bidhaa
zikiuzwa ndani kwa asilimia 70 na ziuzwazo nje ni asilimia 30 pekee.
Aidha kiwanda hicho kinashiriki kwa kutoa bure huduma za kijamii zikiwemo afya, gari la wagonjwa na huduma ya zima moto bure.
Kiwanda
cha tatu kilichotembelewa ni cha Keda Ceremics Limited kilichopo
Chalinze Mikoani Pwani ambacho kinazalisha Tiles ambazo huuza na
kusafirishwa katika nchi za Kenya, Ghana na Senegal.
Akitoa
taarifa ya kiwanda hicho Kaimu Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bruce Ni
amesema kuwa kiwanda hicho chenye uwekezaji wa dola milioni 56 ni
matokeo ya jitihada zilioneshwa na Rais Magufuli na asilimia 30 za
malighafi zinazotumika katika uzalishaji hupatikana Tanzania.
Ni
amesema kuwa mkutano huu umetengeneza fursa kwao na kujenga mahusiano
bora na nchi za Kenya, Rwanda, na Burundi na mipango yao hadi kufikia
mwaka 2026 watakuwa wamelipa kodi kwa serikali zaidi ya dola milioni 12.
Meneja
Masoko na Mauzo Tanzania wa kiwanda cha kusindika matunda cha Elven
Agri company,Brit Bahyare akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe wa
mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao
wametembelea kiwanda hicho jana kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa
na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania.
Afisa
Msimamizi wa kiwanda cha matunda cha Elven Agri ,Martin Leonard Matemba
(kulia) akitoa ufafanuzi mbele ya wajumbe wa SADC waliopata fursa ya
kutembelea kiwanda hicho cha kusindika matunda Elven Agri company
kilichpo wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Msemaji
wa Makampuni ya Motisun Group wamiliki wa Sayona,Aboubakary Mlawa
akiwaonesha wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC box la Juice ikiwa tayari
kusafirishwa maeneo mbalimbali katika kiwanda cha kusindika matunda cha
Sayona kilichopo Mboga - Msoga Chalinze mkoa wa Pwani.
Wajumbe
wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda
wakiangalia namna Juice inavyo sindikwa katiak kiwanda cha Sayona
kilichopo Mboga - Msoga Chalinze mkoa wa Pwani.
Wajumbe
wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda wakikagua
kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo
Chalinze mkoani Pwani
Wajumbe
wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda
wakiendelea kukagua kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya
Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa
Michuzi Tv)
(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...