*Waziri Mkuu asema nchi haina uhaba wa sukari, Kuna viwanda vingi vinavyozalisha sukari Tanzania bara na visiwani Zanzibar

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa amesema kuwa nchi haina uhaba wa sukari kwa kuwa Kuna viwanda vingi zaidi ya vitano vinavyofahamika ambavyo vinapatikana Tanzania bara na visiwani Zanzibar na huzalisha sukari ya kutosha, hayo ameyaeleza leo mara baada ya kutembelea maonesho ya SADC ya wiki ya viwanda na kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na viwanda vya ndani na nje ya nchi ikiwa ni katika kuelekea katika mkutano mkuu wa 39 wa wakuu wa nchi 16 wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika utakaofanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu.

Waziri Mkuu amesema hayo mara baada ya kutembelea maonesho hayo na kusema kuwa maendeleo ni mazuri na washiriki kutoka nchini wamejitokeza kwa wingi na wanaendelea kuonesha bidhaa ambazo nyingi tunazitumia kila siku na huzalishwa katika viwanda vikubwa, vidogo na vya kati pamoja na wafanya kazi za mikono wakiwemo wachoraji na wachongaji na amewataka watanzania kutembelea maonesho hayo na wale wenye hazina ya ardhi na mtaji kuunganisha nguvu na wanajumuiya ya SADC kwa kukaribisha uwekezaji nchini pamoja na kutengeneza masoko ya uhakika na ya kudumu.


Amesema kuwa wananchi waitumie wiki hii katika kwa kuleta mabadiliko nchini kwa kuzingatia kuwa taifa lipo katika mkakati wa kujenga taifa la viwanda;"Wananchi wajitokeze kutangaza bidhaa zao pamoja na kuangalia bidhaa zilizoletwa na makampuni kutoka kwa ndugu zetu wanajumuiya ya SADC na hiyo ni pamoja na kutangaza bidhaa tunazozalisha nchini" Ameeleza Majaliwa 

Aidha amesema kuwa nchi wanachama wameleta bidhaa zao zikiwemo nguo na madawa na wamekuwa wakitembelea katika mabanda ya watanzania na kueleza namna wanavyotumia bidhaa Kama pamba, kahawa na tumbaku katika uzalishaji wao jambo ambalo linatia moyo na kutengeneza fursa ya masoko ya wazi zaidi kwa watanzania.

Mwisho amewataka watanzania kudumisha ukarimu kama ilivyo desturi katika kipindi chote cha ugeni pamoja na kutumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama pamoja na kutembelea vivutio vya utalii.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...