Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani ameeleza kwa kina mkakati wa Serikali ya Tanzania kuhusu namna ambavyo imejipanga kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha, uhakika , gharama nafuu na unaotabirika huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwa kina namna ambavyo wamejipanga kuuza umeme kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC).

Dk.Kalemani amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC ambapo moja ya machapisho hayo yanazungumzia mkakati wa nishati ya meme wa uhakika kwa nchi za jumuiya hiyo katika kuleta maendeleo.

Akifafanua zaidi ,Waziri Kalemani amesema kuwa katika eneo la nishati ya umeme kuna mambo manne makubwa na kwamba jambo la kwanza kama nchi ni kujihakikishia kuwa na umeme wa kutosha kwa ajili ya kuleta maendeleo kupitia uchumi wa viwanda.Mbili umeme unaotabirika, tatu wa uhakika na nne wa bei nauu.

"Kwa sasa upande wa Tanzania kuna mambo matatu likiwemo la makubaliano ya nchi za SADC kwamba kila nchi ijenge miundombinu ya umeme ambayo itaunganisha kati ya nchi na nchi. Kama nchi kwa upande wetu Tanzania tumeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha tunakuwa na umeme wa kutosha lakini wakati huo huo tumeangalia na malengo ya nchi za SADC na katika eneo hilo tumeweka majukumu ya kuzalisha umeme megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025,"amesema Waziri Kalemani.

Amefafanua katika kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha kwa ajili ya kuuza kwa nchi za jumuiya hiyo Serikali imeweka mkakati wa kutumia umeme mchanganyiko ukiwemo wa gesi asili na umeme unatokana na maji."Katika eneo la gesi asilia pamoja na gesi iliyopo , pia tunaendelea kuvumbua gesi na tunazo futi za ujazo trilioni 57 .54 na kati hizo futi za ujazo trilioni 8.8 zitatumika kuzalisha umeme.

" Pia kuna chanzo cha maji na kupitia utafiti ambao umefanyika kwa miaka mitano imeonekana tunaweza kuzalisha mpaka megwati 4,000 na tayari tumeanza na maporomoko ya mto Rufiji ambapo tutatalisha mgewati 2,115.Mradi wa umeme wa maporomoko ya Mto Rufiji ni wa kwanza na wa kihistoria kwa ukubwa nchini Tanzania, ni bwawa la kwanza la kuzalisha umeme Afrika Mashariki, ni bwawa la nne kwa Bara la Afrika na kwa dunia ni kati ya mabwawa 70 makubwa ya kuzalisha umeme mwingi,"amesema Dk.Kaleman.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa mara ya kwanza katika nchi za SADC zimeingia kwenye historia ya kuwa na mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme."Tumeanza na mradi huu wa umeme wa maporomoko ya bonde la mto Rufiji kwasababu tunakwenda kuleta mambo manne ambayo ni ya umeme wa umeme, unaotosheleza, unbaotabirika na gharama nafuu,".

Amefafanua kuwa sehemu ya pili ni kwamba unapokuwa na umeme wa kutosha na gharama na fuu unaweza kusambaza sehemu nyingi na kwa gharama nafuu, hivyo mkakati ulipo ni kujenga miundombinu ya kuusafirisha .

"Kwa sasa katika nchi yetu tunajenga miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye kona zote nne za nchi yetu.Tunafahamu ajenda hapa ni kuzalisha umeme wa uhakika na kusambaza, hivyo ni muhimu kujenga miundomboni ya kusambaza umeme huo,"amesema Dk.Kalemani huku akitaja baadhi ya kona hizo ni ile ya kutoka Dar es salaam kwenda Kaskanini.

Wakati kona ya pili amesema ni kuutoa umeme kutoka Iringa, Mbeya, Sumbawanga, Kigoma mpaka Nyakanazi.Pia amesema kuna mradi wa umeme wa kilovoti 400 ambao unatoka Mkoa wa Iringa kwenda Mbeya ambao unaweza kwenda mpaka nchini Malawi na tayari wamepata fedha kutoka Benki ya Dunia."Makubaliano ya nchi za SADC ni kuuziana umeme kulingaa na mahitaji".

Amesisitiza kuna mkakati wa mradi wa kusafirisha umeme kati ya Zambia ,Tanzania na Kenya na tayari umeshaanza. "Na huu mradi ni muhimu katika kuunganisha umeme kwa nchi za SADC, hivyo mradi wa umeme bonde la Rufuji unatakapokamilika tutauuza kwa nchi nyingine za jumuiya ikiwemo nchi ya Malawi,Zambia na Congo DRC".

Hata hivyo amefafanua kukiwa na umeme wa kutosha maana yake maeneo mengi ya vijiji yatakuwa na umeme wa uhakika na hivyo kutaisaidia kupunguza uharibifu wa mazingira huku akieleza kuna mikakati mbalimbali ya kuhakikisha nishati ya umeme na gesi asili inatumika katika maeneo yote nchini.

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa nchi za SADC kuhakikisha zinaweka mikakati madhubuti ya kuunganisha umeme kwenye maeneo ya vijiji ili kuondoa changamoto ya uharibifu wa mazingira.

WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC ,ambapo moja ya machapisho hayo yanazungumzia mkakati wa nishati ya meme wa uhakika kwa nchi za jumuiya hiyo katika kuleta maendeleo.

Kalemani ameeleza kwa kina mkakati wa Serikali ya Tanzania kuhusu namna ambavyo imejipanga kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha, uhakika , gharama nafuu na unaotabirika huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwa kina namna ambavyo wamejipanga kuuza umeme kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC).
WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani akisalimiana na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya SADC,Dkt . Stragomena Tax kabla ya uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC
WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani (kulia) pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiyasoma baadhi ya majarida kabla uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC 

  WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani (kulia) akimsikiliza wakati akimueleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kabla ya uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC

Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwemo wanahabari wakiwa ukumbini humo kushuhudia uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC .Picha na Michuzi JR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...