Na Moshy Kiyungi,Tabora.


Jina la Wema Sepetu ni maarufu lililojitokeza hususan baada ya kushiriki na kushinda mashindano ya Miss Tanzania ya mwaka 2006.

Aliongeza umaarufu zaidi baada ya kujikita katika tasnia ya maigizo katika filamu mbalimbali.

Pamoja na sifa zote hizo, Wema Sepetu amekuwa nyota asiyefutika kwenye vichwa vya habari vya magazeti ya udaku na mitandao ya kijamii kila mara.


Kabla ya hapo hakuwahi kufikiria katika maisha yake kama angekuja kuwa mmoja kati ya ma-star wakubwa hapa nchini hadi nchi za nje.

Wema ilitokea mpaka siku mmoja akiwa kwenye matembezi yake Slypway Masaki, alikutana na dada Mange Kimambi.Kimambi baada ya kumuona Wema Sepetu alivyo, akamshawishi kushiriki katika mashindano ya Miss Tanzania.

Wema aliukubali ushawishi huo akaamua kushiriki shindano hilo, ambapo aliibuka kidedea akawa Miss Tanzania mwaka 2006, akawagalagaza Jokate Kidote Mwegelo na Lisa Jensen.

Wasifu wa mlimbwede huyo unaeleza kuwa alizaliwa Septemba 28, 1988 akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya mabinti wanne wa marehemu Balozi Isack Abraham Sepetu.

Balozi Sepetu alikuwa Mnyamwezi wa toka mkoani Tabora, aliyehamia Zanzibar miaka mingi ya nyuma.Wakati wa uhai wake Balozi Sepetu aliwahi kuhudumu katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo za Uwaziri na Ubalozi wa Tanzania nje ya nchi.

Mama Wema alikuwa ni mke wa pili, wa kwanza alikuwa mama Amani.
“Kwetu sisi tuko wanne na mimi ndio mtoto wa mwisho, nina dada watatu.
Wa kwanza na wa tatu wako Marekani, wa pili yupo hapa hapa, ameolewa ana familiya yake.

Dada yangu wa kwanza yuko Marekani anafanya kazi, amejaaliwa kupata mtoto mmoja. Wa tatu yuko huko huko Marekani anasoma na anafanya kazi” alisema Wema.

Wema alianza elimu ya msingi na hadi sekondari katika shule moja pekee, iitwayo ‘Academic International’ iliyopo maeneo ya Mikocheni, Dar es Salaam.

Pamoja na yote hayo, binti huyu amelelewa na kuishi kama mtu wa Magharibi (Ulaya).

Wema Sepetu ni mwanamitindo, mjasiriamali na mwigizaji wa Bongo movie kutoka nchini Tanzania.

Kabla ya kuwa Miss Tanzania, alikuwa na mwandani wake japo hakuwa super star.Hawakudumu katika mahusiano yao kwakuwa mara baada ya kushikilia taji la Miss Tanzania, Wema alikuwa na majukumu mengi yaliyokuwa yakimkabiri.

Jambo lililomfanya akose muda wa kukutana na mwandani wake huyo, lakini ni kipindi hicho ambapo alikutana na Steven Kanumba, wakaanza uhusiano mara moja.

Uhusiano wao ulikwenda vizuri, nyota zao zote zikang'aa sana.
Kanumba sasa akaonekana Kanumba wa ukweli, si yule wa kwenye maigizo ya kikundi cha Kaole tena.Wakashirikiana kutengeneza filamu zilizokuwa na ubora wa hali ya juu, zilizozidisha umaarufu wao mara dufu.

Hakuna ubishi kwamba Kanumba ndiye aliyegundua kipaji cha Wema Sepetu, pia ndiye aliyemuibua katika sanaa ya maigizo.Wema kwa sababu alizokuwa nazo mwenyewe, alimsaliti Steven Kanumba, akapata ‘mshikaji’ mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Jumbe.

Tabia za Jumbe hazikuwa nzuri kwa jamii, alikuwa akituhumiwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, yaliyopelekea hadi kuswekwa rumande.
Juhudi kubwa alizifanya mama yake Wema kumnasua binti yake mikononi mwa Jumbe.

Heka heka za Wema wa Sepetu hazikuishia hapo akajikuta yuko mikononi mwa mwanamuziki Chalz Baba.Wazazi wa Wema baada ya kaona binti yao anapamba magazeti kwa habari mbaya, wakaamua kumpeleka nchini Marekani kwa mmoja wa dada zake, wakiwa na matumaini ya kubadilika kitabia.

Akiwa huko alikuwa anachati na watu kwa kutumia mitandao ya kijamii, chating ya kwanza ya Wema na Diamond ilikuwa kwenye Facebook.
Baadaye Wema Sepetu alirejea nchini akapanga nyumba na kumkaribisha mpenzi wake mpya Diamond Platnumz, wakaanza maisha ya pamoja kwa raha na mstarehe.

Baadhi ya watu walipigwa na butwaa kila mmoja akilalama kwanini Wema anamchukua mtu kama Diamond, asiye na mbele wala nyuma na mengi mabaya juu yao.

Ujasiri wa Wema uliweza kukomaza penzi lao baada kuweka pamba masikioni kwa yasemwayo na watu.Alitaka kudhihirisha kuwa Naseeb Diamond aliyempenda yeye, ni ‘Almasi’ ambayo inang'aa duniani kote.
Wakati huo Diamond Platinum alishatoka na nyimbo zake kama mbili hivi kali moja wako wa Mbagala.

Lakini hakuwa juu kiasi hicho na bila Wema. Yaelezwa kuwa Diamond angebakia kama wasanii wengine wanatesa na nyimbo kali ila nyota hazing'ai kivileee Ben Pol, Chid Benzi Barnaba na wengineo.

Wema Sepetu hakuona soni kuonesha pendo lake kwa Diamond popote wawapo, alidiriki kumpa mabusu mbele ya kadamnasi, maneno ya watu hayakuwastua wakazidisha mapenzi mara dufu.

Ndipo watu wakaanza kumuona Diamond akiwa katika muonekano wa pili, aling'aa sana akawa na swaga za Wema, Kiingereza kidooogo.

Baadhi ya mwanamke wakatamani wawe kama Wema na Diamond.

Wawili hao wakawa simulizi tamu midomoni mwa watu ukizingatia Wema anavyojua kudeka na kupenda, watu wakachanganyikiwa na mapenzi yao yalivyokuwa yamenoga.

Wema alimpenda kwa dhati Diamond japo alipigwa vita sana na jamii kuwa hafai eti si wa hadhi yake!

Lakini hakuvunjika moyo alimpenda zaidi Diamond nakutufanya watanzania wote na ulimwengu wote kumtambua Diamond na kipaji chake na hadi akaonekana kijana mtanashati, hadi kufikia leo hii amekuwa super star.



Wema aliwahi kuvalishwa pete ya uchumba na

Diamond Platnumz, baadaye uchumba ukapotelea mbali.



Kipaji zaidi cha Wema kiligundulika katika sanaa ya filamu, ambapo alifanikiwa kucheza vema kabisa katika filamu A Point of No Return, akishirikiana na mchezaji filamu maarufu wa Kitanzania Steven Kanumba.




Wema Sepetu amezidi kupata umaarufu japo magazeti mengi yakiendelea kumchafua usiku na mchana.

Licha ya fitna hizo, Wema ambaye kama akitamka kuwa leo atakuwa Jangwani ku-perfom, anayetaka kumuona aje, pasipo shaka maelfu ya watu watakusanyika.

Inaaminika kuwa nyota yake imepelekea kila atakaye mshika mkono, naye lazima awe juu na hii si kwa wanaume wake pekee bali hata mashoga zake wa kike mfano halisi ni Snura.


Pamoja na Wema na kusalitiwa mara nyingi na kusemwa vibaya na mashoga zake, bado yuko juu, anamiliki Kampuni yake ya Production inayoitwa Endless Fame.

Pia anakipindi chake ambacho hivi karibuni kinategemewa kurushwa hewani kitakachoitwa Reality Show, anamiliki nyumba na magari kadhaa.

Mlimbwende huyo anajiweza kimaisha na Mungu anazidi kumbariki kwani anajitoa sana kwa watu na mtoaji mzuri wa sadaka.

Kila la heri Wema Isack Sepetu.

Mwisho.

Habari hizi zimeandaliwa kwa msaada mkubwa wa mitandao.

Mwandaaji anapatikana kwa namba: 0784331200, 0713331200, 0736331200 na 0767331200.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...