Meneja wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) mkoa wa Ilala, Mhandisi Sotco Nombo (katika) na Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Mhaji.walimpotembelea Hamad Awadh nyumbani kwake Majumba Sita, Ukonga jijini Dar es Salaam. Hamad kwa sasa anapumua kwa kutumia Mashine ya Oxygen na Gesi anahitaji Msaada kupatiwa matibabu nchini India.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) limetoa msaada wa kiasi cha fedha Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya matibabu na Mita (Luku) yenye umeme wa miezi sita sawa na Tsh Milioni Moja na Nusu kwa Kijana Hamad Awadh anayesumbuliwa na tatizo kupumua.

Akizungumza baada yakumtembelea Hamad nyumbani kwake, Majumba Sita, Ukonga jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Mhaji amesema kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Tito Mwinuka wameguswa na hali ya Hamad yakupumulia Oxygen.

Leila amesema kutokana na matumizi makubwa ya Umeme kwa Mashine yake anayotumia kwa ajili yakupumua, wameona wamsaidie Mita ya peke yake, tofauti na wapangaji wenzake anaoishi nao nyumba moja.

‘’Hamad ni Mtanzania mwenzetu ambaye alikuwa na shughuli zake anafanya kama kawaida, lakini kutokana na maradhi yanayomsumbua ameshindwa kuendelea na kazi zake, Sisi kama TANESCO tumeliona hili hatuwezi kumuona Mtanzania mwenzetu anateseka hivi’’, amesema Leila.

Naye, Meneja wa Shirika hilo mkoa wa Ilala, Mhandisi Sotco Nombo amesema Shirika hilo limeguswa na hali hiyo ndio maana linamsadia kwa hali na mali, Hamad Awadh.

‘’Rais wetu anasisitiza Watanzania tuwe Wazalendo, sisi kama TANESCO tuemona tulibebe hili la Hamad kama Watanzania ili tumsaidie’’, amesema Mhandisi Sotco.

Hamad Awadh ambaye kwa sasa anataka msaada kwa ajili yakupatiwa matibabu nchini India, ameshukuru kwa msaada huo kutoka TANESCO, amesema kwa sasa maisha yake ni umeme na endapo utakatika basi huwa anatumia Gesi, ameshukuru Hospitali ya Mloganzila kwa huduma walizompatia mpaka kufikia hatua hiyo.

‘’Nasema kila siku moyoni mwangu, hata siku nikidondoka Mloganzila Hospital wamenifanyia kitu kama Mtoto wao, naishukuru pia Serikali kwa huduma zake, naomba sio ninyi tu (TANESCO) na wengine wakisikia kilio changu basi naomba msaada wao'', ameeleza Hamad.

Kwa upande wake Abdul Athumani, Mjomba wa Hamad amesema changamoto kubwa kwa Hamad ni Umeme kutokana na kutumua Oxygen inayotumia zaidi umeme, amesema gaharama nyingine ni Gesi wanayotumia kwa Mgonjwa huyo inayonunuliwa Elfu 45 kila mwezi hivyo wanaomba msaada.

Ugojgwa wa Hamad Awadh ulianza mwaka mmoja na nusu uliopita baada yakupata homa ambapo ilipelekea kupelekwa Hospitali ya Amana, Ilala baadaye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo ilibainika Mapafu yake yamesinyaa na Moyo wake umehama kutoka kulia na kwenda kushoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...