Muwezeshaji Andrew Michael Mwaselela kutoka taasisi ya Fursa Connect Initiative akitoa somo Kwa wajasiliamali vijana kutoka katika kata za Makumbusho, Kijitonyama na Mwananyamala katika semina liliyofanyika Kibamba.

VIJANA wa wilaya ya Kinondoni wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo ya fedha zinazotengwa kwa ajili yao ili wajiajiri kwa kuanzisha na kuendeleza biashara za ujasiriamali waondokane na umaskini.


Akizungumza katika semina ya siku mbili ya Ujasiriamali iliyoandaliwa kwa ajili ya vijana kutoka kata tatu za Makumbusho, Kijitonyama na Mwananyamala, Afisa Maendeleo ya Jamii na Vijana kutoka Manispaa ya Kinondoni Bi Halima Chodry Kahema amesema vijana wengi wanakuwa wanaoga kuomba mikopo hiyo inayotolewa kwa masharti nafuu.

Vijana wa kiume ndio wanaokwepa zaidi mikopo hiyo, ukilinganisha wa wasichana, imeelezwa.

“Halmashauri inatenga sehemu ya mapato yake kwa ajili ya kuwakopesha vijana ili wajiajiri waondokane na umaskini,”

“Lakini, kuna kipindi fedha hizi huwa zinabaki kwa sababu ni vijana wachache wanajitokeza,” amesema Kahema, huku akiongeza kuwa kuna vijana, licha ya kuchukua mikopo, wanakuwa hawana nidhamu ya pesa wanayokopeshwa, huku akiwashauri kupata mafunzo ya ujasiriamali ili kutimiza malengo yao ya biashara.

Ameishukuru asasi ya Pakacha Group, iliyoandaa semina hiyo kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society, akisema wanaisaidia serikali kwa kuendana na falsafa ya mheshimiwa Raisi John Pombe Magufuli ya kuwataka vijana wawezeshwe kiuchumi.

Muwezeshaji Andrew Michael Mwaselela kutoka katika taasisi ya Fursa Connect Initiative amesema vijana wengi, hasa wale wasomi kutoka vyuoni ndio wanakuwa waoga zaidi, wakiamini wanahitaji mtaji mkubwa kuanzisha biashara, badala ya kuifanyia kazi ile dhana ya ujasiriamali inayosema ‘Fikiri zaidi, Anza kidogo’.

Amesema ujasiriamali una faida nyingi, kama vile kuendeleza uchumi binafsi, uchumi wa familia na uchumi wa nchi.

Ameongeza ili mtu awe mjasiriamali mzuri, inabidi aangalie fursa za kibiashara, awe na mtaji (kutunza na kukuza), awe mbunifu, awe na mawasiliano na wateja na kutoa huduma bora kwa wateja wapya na wale wa zamani.

Katibu wa Pakacha Group, Haroun Jongo amesema wanategemea kuandaa semina kama hizo katika siku za usoni ili kufungua fursa nyingi za ujasiriamali kwa vijana, huku akiwashukuru The Foundation For Civil Society kwa ufadhili wenye lengo la kusaidia vijana waondokane na umaskini kwa maslahi ya taifa.

Mmoja wa wajasiriamali, Martin Bogwe kutoka kata ya Mwananyamala anayejishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa pilipili ya mbilimbi anasema fursa zipo nyingi , akiwataka vijana kuzichangamkia ili kuondokana na utegemezi.

Zaidi ya vijana wajasiliamali wapatao 60 wanaojishughulisha na ujasiliamali walishiriki katika semina hiyo, ambayo pia maafisa maendeleo kutoka katika kata za Makumbusho, Mwananyamala na Kijitonyama walishiriki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...