Na Rhoda Ezekiel, Kigoma


WANANCHI wilayani Kakonko mkoani Kigoma wameshauriwa kuacha kwenda kwenye shughuli za Kilimo wakati wa uchaguzi ili kufika katika vituo kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo na kuepuka kuchaghuliwa viongozi wanaotafuta uongozi kwa matakwa yao binafsi.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, wakati akiwahamashisha wananchi hao kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu na kuhakikisha kuwa wanachagua viongozi waadilifu, wasiopenda rushwa bali wapenda maendeleo na kuimarisha ulinzi na usalama wa eneo analoliongoza.

Amesema kumekuwa na wananchi wengi Vijijini kutoshiriki katika chaguzi mbalimbali hususani wakati huu msimu wa Kilimo ambapo wananchi wengi wanahamia mashambani; hivyo wananchi wanapaswa kutenga muda wao wa kushiriki katika kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi mbalimbali katika uchaguzi huo, na ili shughuli wanazozifanya ziweze kuwaletea maendeleo lazima kupata viongozi wazuri.

Aidha, ameeleza kuna baadhi ya viongozi wa vijiji vilivyoko mpakani wanajihusisha na vitendo rushwa kwa kugawa ardhi kwa wananchi ambao inasadikia siyo raia wa Tanzani na kushiriki kuhifadhi mifugo yao na pia kuwanyanyasa wannanchi.

Yote yametoke kwa kuwa wananchi hawakujipanga kujua ni nani kiongozi atakae waongoza kwa misingi ya uzalendo na uadilifu. 

" Nitoe mwito kwenu Wananchi ni haki ya kila raia kushiriki katika uchaguzi iwe kuchaguliwa au kuchagua; na tutakapo jitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi itatusaidia kupata viongozi watakao tuongoza katika Misingi ya uadilifu na uwajibikaji, ni jukumu letu kuhakikisha uchaguzi huu tunatenda haki, tuhudhurie mikutano ya wagombea na tusikilize sera zao ili kujua ni kiongozi gani anatufaa,'amesema.

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Masumbuko Magang'hila aliwataka wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ilikuweza kushiriki kikamilifu katika kuchagua viongozi.

Amesema daftari hilo litahusisha wale ambao hawakujiandikisha katika daftari la awali la kupigia kura, waliofikia umri wa kupiga kura, waliopotelewa vitambulisho vyao na waliohama makazi yao ya mwanzo na kuhamia sehemu ambayo hawakujiandikishia.

Alieleza kuwa uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu na watakaoshiriki ni wale waliojiandikisha, na wale ambao wanasifa za kugombea na kuwataka Wananchi wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali na wasiogope.

Kwa upande wake Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Kakonko, Ladisraus Ibrahim msaki Aliwataka Wananchi kutoa taarifa kwa yeyote atakaye kuwa anajihusisha na vitendo vya rushwa kwa ajili ya kupata uongozi ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria na kuepuka kupata viongozi wasiofaa watakao kuwa wapenda rushwa na wasiopenda maendeleo.

Nao baadhi ya Wananchi walikuwa na maoni tofauti juu ya uchaguzi, Joackim Antony ni mkazi wa kijiji cha Kabingo alisema Wanatambua ni haki ya kila mwananchi kushiriki katika uchaguzi na wao kama vijana watahakikisha wanashiriki kikamilifu kuhakikisha wanapata viongozi walio bora.

Amesema changamoto ambayo inayowakatisha tamaa ni pale wao wanapochagua viongozi harafu wanajitokeza baadhi wanawapitisha wagombea wanaowataka wao bila kushinda hivyo wanaiomba serikali kuwa makini katika uchaguzi huu ili kuweza kuondokana na changamoto hizo.

Mwananchi wa kijiji Kabingo Nezia Kasiano amesema atahakikisha wanashiriki katika uchaguzi huo na kwamba hakuna jambo litakalo wazuia kushiriki, endapo watapata viongozi wazuri itawasaidia hata kupanga mipango ya maendeleo katika vijiji vyao
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Wananchi hao 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...