BENKI ya NBC imeendelea kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja kwa kufanya matukio sehemu mbalimbali nchini na hapo jijini Dar es Salaam ikitoa elimu kuhusu umuhimu wa bima na pia ikiwaleleza wateja aina mbalimbali ya huduma za bima zitolewazo na benki hiyo.
Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Kitengo cha Bima wa NBC, Benjamin Nkaka alisema watanzania wanapaswa kuwa utamaduni wa kujiwekea bima wao pamoja na watoto wao dhidi ya matukio na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza wakati wowote.
Akitoa mfano wa bima hizo ni bima ya elimu ya Educare itolewayo na inayomuwezesha mzazi kuweka akiba kidogokidogo kwa ajili ya elimu ya mtoto wake pindi yatokeapo majanga yanayoweza kusababisha ulemavu wa kudumu ama kifo.
“Tumekwishakuwa na huduma hii, tunachotaka sasa ni kwa wateja kuweza kuielewa vivuri, na ndio maana tumendaa hafla kama hii ili kuwafahamisha wateja wetu na wananchi kwa ujumla huduma ya bima ya elimu ya NBC inavyoweza kumkomboa mteja,” alisema.
Alisema kwa kupitia huduma hii mteja humwekea akiba mtoto wake kidogokidogo kwa kiasi atakachopanga kwa mkataba wa muda kuanzia miaka saba hadi 18 ili kugharamia elimu ya mtoto wake.
“Bima hii ya elimu ni mpango ambao mzazi huweka akiba kila mwezi hivyo kuleta faraja moyoni kwamba endapo chochote kitatokea iwe ulemavu wa kudumu ama kifo kabla ya muda huo basi bia itagharamia elimu ya mtoto wako.
“Kiwango cha chini ni miaka saba hadi 18 na kiwango cha chini cha kuwekeza katika mpango huu kwa mwezi ni shs 7,500/- hakuna kiwango cha mwisho cha juu. Uwekezeji katika elimu ya mtoto ni jambo pekee katika kuhakikisha malengo ya kielimu ya mtoto yanatimia ,” aliongeza Bwana Nkaka.
Ofisa
wa Bima wa Benki ya NBC, Catherine Ngowi (kulia) akitoa
elimu ya masuala ya bima n aina mbalimbali ya huduma za bima zitolewazo
na NBC kwa ammoja wa wateja wa benki hiyo, Miryam Mjema ikiwa ni moja
ya matukio katika
kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo mjini Dar es Salaam
hivi
karibuni. Wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bima wa benki hiyo,
Benjamin
Nkaka na ofisa mwingine wa NBC, Batuli
Kassim.
Ofisa wa Bima wa benki ya NBC, Emarynziana Mtega (kulia),
akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kujiwekea bima na aina mbalimbali ya huduma za
bima zitolewazo na NBC kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo kutoka Kampuni ya Mogas Tanzania
Ltd, Grayson Kazeni kiwa ni moja ya matukio katika kuadhimisha Mwezi wa Huduma
kwa Wateja wa benki hiyo mjini Dar es Salaam hivi karibuni.
Maofisa wa benki ya NBC, wakizungumza na wateja wakati
wakitoa elimu kuhusu masuala ya bima kwa wateja ikiwa ni moja ya matukio ya
maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakipozi kwa picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo. Wafanyakazi hao walitoa elimu ya bima ikiwa ni pamoja na bidhaa mbalimbali za bima zitolewazo na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...