Na Shushu Joel

KATIBU tawala wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Kasilda Mgeni amefurahishwa na wananchi wa halmashauri ya chalinze kwa kuweza kuitikia wito wa kujiandikisha kwenye daftali la kupiga kura.

Wananchi wamekuwa mstali wa mbele katika zoezi la kujiandikisha kutokana na uelewa wa kutumia fursa ya kuwachagua viongozi wao.

Akizungumza na baadhi ya wananchi katika moja ya vituo vya kujiandikishia alivyotembelea kwenye kata ya ubena,halmashauri ya chalinze katibu tawala huyo aliwapongeza wananchi waliojiandikisha na kuwataka wawahamasishe na wenzao ambao bado ili nao wajiandikishe kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mtaa na vitongoji unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi na moja.

"Kwa kweli chalinze wananchi hongereni sana kwa kujiandikisha kwa wingi nadhani kufikia mwisho wa zoezi hili mtakuwa mmevuka lengo lenu" Alisèma.Aidha Mgeni amempongeza mbunge wa jimbo la chalinze mh Ridhiwani Kikwete kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhamasisha wananchi wake ili wakajiandikishe.

Aliongeza kuwa Kikwete ni kiongozi wa pekee aliyefanikisha kazi ya hamasa kwa wananchi kwani watu wamejitokeza na wanazidi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiandikisha na kwa baadhi ya vituo kuonekana wamemaliza kuandikisha huku wakiwa wamevuka malengo yaliyokuwa yamekusudiwa.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema kuwa ujio wa kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na katibu tawala imemuongezea nguvu na mzuka zaidi.

Alisema kuwa wananchi wa chalinze wamehamasika wenyewe mara baada ya kutangaziwa na gari maalum lililotolewa na halmashauri kwa ajili ya kuwahamasisha wakazi wa chalinze kuweza kujitokeza.Aidha Aliongeza kuwa kila kazi inachangamoto zake lakini kwa chalinze changamoto kubwa ni mfululuzo wa mvua zilizokuwa zikinyesha hivyo kupelekea wananchi kutojitokeza huku wengine wakiwa mashambani. 

"Kwa jinsi hali inavyoelekea wanachalinze tutavuka malengo tuliyokuwa tumejiwekea kwani kwa sasa tuna zaidi 80% huku siku chache zikiwa zimebaki.Naye msimamizi mkuu wa uchaguzi katika halmashauri hiyo Shabani Milao amempongeza mbunge kwa jinsi alivyojitolea kutoa hamasa kwa wananchi katika zoezi zima la kujiandikisha.

Aliongeza kuwa zoezi linaenda vizuri na kile kichokuwa kimekusudiwa na serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...