Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaamuru  washitakiwa tisa wanaokabiliwa na kesi ya wizi wa katoni 700 za korosho kulipa fidia ya Sh.milioni 125 kama hasara waliyoisababisha kwa Serikali.

Washitakiwa hao ni  Robert Slaa, Isihaka Ngubi, Cathbert Mlugu, Mrisho Mindu, Mauridi Haji, Hamza Bunda, Kelvin Ngwandu, Joseph Robert na Joseph Mihayo wamesomewa adhabu hiyo leo Oktoba 23,mwaka 2019 baada ya kuomba msamaha na kukiri makosa yao.

Akisoma adhabu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi amesema washitakiwa wote wataachiwa huru kwa sharti la kutofanya kosa lolote kwa muda wa mwaka mmoja pia amewataka watimize masharti ya  makubaliano yanayowataka kulipa hasara ya korosho walizoiba.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Januari 26 hadi Februari 6, 2018 katika yadi ya Kampuni ya Zambia Cargo and Logistics Limited, waliiba katoni 700 za Korosho zilizobanguliwa zenye thamani ya Dola za Marekani 54,180 sawa  na zaidi ya Sh.milioni 125.

Ilielezwa kuwa korosho hizo zilikuwa mali ya Barabara Trading Tanzania Limited na zilikuwa zikisafirishwa kwenda nchini Vietnam.

Ilidaiwa washitakiwa waliiba katoni hizo za korosho zilizokuwa katika kontena na kisha kuyajaza mchanga na mengine kuyaacha matupu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...