Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji(wa pili kulia) akikabidhi tuzo ya Kampuni Bora DSE kwa mwaka 2019 katika sekta isiyo ya Viwanda, kwa Mkuu wa Uhusiano wa Uwekezaji na Miradi Maalumu wa Vodacom Plc, Robin Kimambo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa na AfisaMtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Usalama wa Mitaji, Nicodemus Mkama. Hafla hii ilifanyika juzi jijini Dar Es Salaam.



Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania, Vodacom imeshinda tuzo ya soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika juzi jijini Dar es Salaam, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Mazingira, Jamii na Utawala Endelevu’ Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu K. Kijaji.

Lengo kuu la tuzo hizi ni kukuza ubora wa biashara katika nyanja ya Utunzaji wa Mazingira, Utawala Bora wa Kampuni, Kuongeza Uwajibikaji katika shughuli za Kijamii na kuhakikisha kuwa DSE inaendelea kutimiza wajibu wake kwa wanachama.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkuu wa Uhusiano wa Uwekezaji na Miradi Maalumu wa Vodacom Plc, Robin Kimambo, alisema tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa kampuni hiyo ambayo kwa sasa inaongoza kwa uvumbuzi kwenye teknolojia ya mawasiliano nchini.

“Jambo la msingi ni kuwaahidi watanzania kuwa, tutaendelea kuwa wabunifu na wavumbuzi ili kuendelea kutoa huduma ambapo kwa sasa tuna takriban wateja zaidi ya milioni 14 nchi nzima,” alisema.

Washiriki wa tuzo hizo ni kampuni zilizoorodheshwa DSE ambazo ni pamoja na Madalali au Wafanyabiashara, Washauri waliopendekezwa pamoja na vyombo vya habari vya kidigitali na magazeti.

Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc iliorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam Agosti 15, 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...