Kaimu Mkuu wa kitengo cha huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha akizingumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma ya kutoa fedha kwa njia ya ATM, pembeni yake ni Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch,Company Ltd, Danford Mbilinyi, uzinduzi huu umefanyika leo Dar es salaam.
Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch,Company Ltd, Danford Mbilinyi, akifafanua Jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma ya kutoa fedha kwa njia ya ATM .Uzinduzi hum umefanyika katika makao makuu ya Tigo Jijini Dar Es salaam.
Kaimu Mkuu wa kitengo cha huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha akifanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati akizindua huduma ya kutoa fedha kwa njia ya ATM, pembeni yake ni Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch,Company Ltd, Danford Mbilinyi, uzinduzi huu umefanyika leo Dar es salaam

Kaimu Mkuu wa kitengo cha huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha akizindua huduma ya kutoa fedha kwa njia ya ATM, pembeni yake ni Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch,Company Ltd, Danford Mbilinyi, uzinduzi huu umefanyika leo Dar es salaam


 Tigo kupitia kitengo cha Tigo Pesa imeingia ubia na taasisi ya UmojaSwitch (BCX) kuzindua huduma ya kutoa fedha kwa njia ya ATM ambayo ni rahisi na ya uhakika kwa wateja wa Tigo.

Ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ni hatua muhimu katika kuchochea agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kwani inaifanya huduma ya Tigo Pesa kuwa zaidi ya huduma ya kifedha kwa njia ya simu na kuwa huduma ya kibenki.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, Kaimu Mkuu wa kitengo cha huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema huduma hiyo mpya ni utekelezaji wa mkakati wa Tigo wa kutoa huduma za kidigitali zenye ubora ili kukidhi mahitaji ya wateja.

“Tuna furaha kuzindua huduma hii mpya ya kibenki ambayo itawapa wateja wetu uhuru wa kifedha kwakuwa ni njia rahisi na ya haraka ya kupata pesa mahali popote kupita ATM za UmojaSwitch zilizopo maeneo mbalimbali ya nchi,” alisema Pesha.

Pesha alisema huduma hiyo mpya itarahisisha utumaji na kupokeaji wa pesa kwa kutumia ATM za UmojaSwitch zaidi ya 350 zilizopo hapa nchini hivyo kuchochea ustawi wa kiuchumi kwa wateja wa Tigo.

“Ni matumaini yetu kuwa huduma hii itachochea utekelezaji wa lengo letu la kuwafikia wananchi kila kona ya nchi na zaidi kuchangia agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi.Kwa ushirikiano huu Tigo inakuza mtandao wake kwa kuwapa wateja njia mbadala ya kutoa fedha zilizoko kwenye akaunti ya Tigo Pesa kupitia ATM za UmojaSwitch.Hii inasaidiwa zaidi na mawakala zaidi ya 100,000 waliopo nchini,” alisema.

Mteja wa Tigo atatakiwa kufuata hatua zifuatazo kwa ajili ya kuweza kutoa fedha kutoka katika ATM za benki ya UmojaSwitch, ata Piga *150*01, Chagua 7. Huduma za Kifedha, Chagua 5. Kutoa pesa ATM,Chagua Benki, alafu ataandika Kiasi cha fedha anachotaka kutoa kisha namba yake ya siri.Katika ATM, mteja atabonyeza kitufe cha TigoPesa alafu ataingiza namba ya simu, kisha OTP(namba ya siri ya kutumika mara moja tu), halafu atapata fedha zake kutoka kwenye ATM.

Pia, huduma hiyo mbali na kuongeza urahisi wa upatikanaji wa pesa pia itasaidia katika ukuzaji wa sekta ya fedha pamoja na kurahisisha ufanyaji wa miamala muda wowote.

Naye, Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch,Company Ltd, Danford Mbilinyi alisema “ushirikiano huu utachochea ukuaji wa sekta ya fedha huku ukirahisisha upatikanaji wa huduma kwa watu wote kila mahali,” alisema.

Alisema UmojaSwitch ina farijika kushirikiana na Tigo ili kuwapatia wateja uhuru wa kifedha muda wote na zaidi kuokoa muda na gharama kwani ATM za UmojaSwitch zipo maeneo mengi ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...