Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amewataka viongozi wa vyama vya msingi (Amcos) kuacha vitendo vya ubadhilifu na utoaji wa vyeti hewa katika msimu huu wa Korosho
Akizungumza na Viongozi wa vyama vya msingi amesema wao wamekuwa ni chanzo Cha vyeti hewa.
"Sitaki kusikia vyeti hewa anayeleta mzigo wake ndiye anayepaswa kulipwa na si vinginevyo,hatutawavumilia hatua kali tutawachukulia,wakulima wapewe haki zao,"amesema Waryuba
Amesema viongozi ili waweze kuitenda kazi hii kwa weledi ni lazima wapate makarani waaminifu ambao wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi
Hakikisheni makarani wenu wawe na mkataba na wadhaminiwe na watu wenye dhamana hatutaki makarani wababaishaji,"amesema Waryuba
Aidha aliwataka wakulima kukausha korosho zao ili waweze kupata kilo sahihi wanapopeleka ghalani
"Wakulima kausheni vizuri korosho ili zinapokwenda ghalani ziwe na kilo sahihi,mnapopeleka korosho hazijakauka vizuri zinapokaa zinakauka hivyo zinapokuja kupimwa Tena zinaonekana zimepungua utata unaanzia Hapo,"anasema Waryuba.
Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba akifafanua Jambo kwa viongozi wa Amcos
Afisa Ushirika wa Wilaya Sudi Rajabu.
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kikao hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...