Na Woinde Shizza Globu ya jamii ,Arusha 

Vijana wa shule ya sekondari Musa, halmashauri ya Arusha, wameweka wazi kuwa, uelewa mdogo wa jamii hasa wazazi juu ya afya ya uzazi kwa vijana, imekuwa ni chanzo cha mimba na ndoa nyingi za utotoni.

Wakizungumza wakati wa mdahalo wa Afya ya uzazi kwa vijana, uliofanyika shule ya sekondari Musa, mdahalo uliohusisha wanafunzi wote wa shule hiyo, wamesema kuwa, licha ya changamoto nyingi zinazowakabili vijana, bado uelewa mdogo wa vijana juu ya afya ya uzazi, umesababisha ndoa za utotoni na vijana kujikuta kwenye changamoto nyingi za kimaisha.

Wamefafanua kuwa, mara nyingi vijana hushauriana wao kwa wao, juu ya mabadiliko yao ya kimwili yanayoambatana na kuanza mahusiano ya kimapenzi, kwa kupeana taarifa zisizo sahihi, jambo ambalo husababisha mimba zisizotarajiwa pamoja na ndoa za utotoni.

Wameongeza kuwa, kutokana na mila na desturi za jamii zao, inaonesha wazi kuwa, hata wazazi hawana uelewa wa kutosha juu ya afya ya uzazi kwa vijana pamoja na mabadiliko ya kimwili kwa vijana jambo ambalo linasababisha vijana kubaki njia panda na pengine kushindwa kufikia malengo yao kwa kukatiza ndoto zao.

Wanafunzi hao wakwenda mbali zaidi na kusema kuwa, endapo wazazi wangekuwa na uelewa sahihi, juu ya afya ya uzazi kwa vijana, wasingewalazimisha wasicha kuolewa wakiwa na umri mdogo kwa kuhofia wasichana hao kupata mimba kabla ya ndoa.

Kadhalika katika mdahalo huo, vijana walipata fursa ya kujadili kwa kina juu ya afya ya uzazi na changamoto za mabadiliko ya kimwili zinazosababisha mihemko na namna ta kukabiliana na hisia.

Hata hivyo, halmashauri ya Arusha kupitia mradi wa TCI - TUPANGE PAMOJA , unaotekelezwa na shirika la JHPIEGO - Tanzania, wameanzisha huduma Rafiki kwa Vijana, huduma zinazotolewa bure kwenye zahanati na vituo vya afya na kuwataka vijana kwenda kwenye zahanati kupata elimu zaidi juu ya afya ya uzazi kwa vijana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...