Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wadau wa amani na viongozi wa dini kuhubiri suala la amani sambamba na kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili katika jamii ikiwemo udhalilishaji, ubakaji na
matumizi ya dawa za kulevya.

IGP Sirro ameyasema hayo leo akiwa kisiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi
ambapo amewataka wananchi na wadau wa amani kushirikiana kwa pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuifanya nchi kuwa salama.

Kamishna wa Polisi Zanzibar Mohamed Hassan ameeleza kuwa, suala la
kutunza amani ni jukumu la kila mmoja na kwamba ni vyema wananchi kwa
pamoja wakashirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kuhakikisha suala la usalama linazidi kuimarishwa.

Naye Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Mussa Ali Mussa amesema kuwa, viongozi wa dini ni daraja kati ya waumini na Mwenyezi Mungu daraja ambalo viongozi wengine hawana.

Hivyo amewataka viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali kuendelea
kuhuisha Kamati za Ulinzi na Usalama katika nyumba za ibada.

Naye askofu wa kanisa la Kianglikana Dk. Michael Hafidh amesema kuwa,
wamejipanga katika kuendelea kuhubiri amani kwa waumini wao hili kuisaidia jamii kuacha kujihusisha na uvunjivu wa amani na kwamba kwa upande wa viongozi wa dini anayetaka kujihusisha na masuala ya kisiasa ni vyema akaachana na kujificha kwenye kivuli cha dini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...