Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

WAZEE wa Baraza  katika kesi ya tuhuma za mauaji inayomkabili mwanamama Esther Lymo (47) anayedaiwa kumuua mtoto wa dada yake, Naomi John (7) wameishauri Mahakama Kuu kumtia hatiani mshtakiwa kwa mauaji ya kukusudia.

Mahakama Kuu liyoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba 7,2019 imeelezwa hayo na wazee watatu wa baraza wakati wa majumuisho ya kesi hiyo baada ya mashahidi tisa wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi mbele ya Msajili, Pamela Mazengo huku mshtakiwa alileta mashahidi watatu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wazee hao wa walitoa maoni yao kwamba kutokana na ushahidi wa Andrew John (9) ambaye alishuhudia tukio la kupigwa kwa marehemu Naomi John inaonesha wazi mshtakiwa alikusudia kufanya mauaji.

Walidai watoto walikuja Dar es Salaam kwa ajili ya kusoma lakini malengo hayo hayakutekelezeka kwa sababu watoto Naomi na Andrew hawakupelekwa shule matokeo yake walikutana na huo ukatili wa kuteswa na kunyanyaswa na mshtakiwa ambae alikuwa mama wa ubatizo wa mtoto Naomi (marehemu)

Wamedai, kulingana na ripoti ya daktari iliyoonesha marehemu alikutwa na majeraha mwilini huku mshtakiwa mwenyewe alikiri kuwa alimchapa kwa fimbo ya mpera, hivyo inaonesha wazi kuwa aliua kwa kukusudia.

Moja ya ushahidi wa upande wa mashtaka ulidai kuwa, mshtakiwa alimpiga marehemu, kumng'ata mwilini na kisha kumwagia maji ya moto ya chai ambapo inadaiwa ilikuwa tabia yake kuwafanyia ukatili watoto hao Andrew na marehemu Naomi.

Katika utetezi wake mshtakiwa huyo ameiomba Mahakama imuonee huruma na kumuachia huru  huku akidai alikuwa akimchapa marehemu kwa kumkanya na kwamba vidonda na makovu aliyokutwa nayo mwilini alitoka nayo kijijini kwao mkoani Kilimanjaro sababu alikuwa anachunga mbuzi.

Akielezea jinsi namna marehemu Naomi na Andrew John wanavyomuhusu alidai ni watoto wa dada yake na aliwachukua kuishi nao baada ya kuombwa awasomeshe  kwa kuwa dada hakuwa na uwezo ambapo aliishi nao nyumbani kwake Tuangoma Kigamboni kwa takribani miezi 10.

Ambapo alikaa na watoto hao kwa miezi hiyo 10 nyumbani kwake Twangoma mbako pia kuna mapori kama kijijini kwao  Moshi.

"Watoto hao ni watundu sana, huwa wanakimbizana na kucheza vichakani ambako huku nako kuna mapori kama kilimanjaro hivyo ndio maana mwili wake ulikuwa na vidonda na makovu, sijamuua Naomi, nilikuwa nawapenda , naomba Mahakama iniachie huru.

"Machi 25, mwaka 2016 wakati natoka kufanya usafi Saloon kwangu,  nilielezwa na Andrew kuwa Naomi ameamka, amejikojolea yupo barazani. Nilipoingia ndani nilimwambia Naomi akapige mswaki, lakini aliendelea kukaa barazani , Andrew akaniambia tena hapigi mswaki anachezea maji, nikaongea kwa sauti kwamba nikitoka ndani nitàmchapa, nilipotoka Naomi akakimbia nikamwambia Andrew amkamate.

" Alipoletwa nilichuma fimbo katika mti wa mparachichi na kumchapa kwa nia ya kumkanya kama mzazi, wakati namchapa Naomi akasema amechoka, mi nilizani ni utani kwasababu ya kukimbia na ujeuri wake, nilimnyànyua na kumweka barazani, nikaenda kutafuta dawa, nilivyorudi nilikuta amelegea sana, nikachukua gari ya jirani na kumpeleka hospitali Temeke amapo daktari alitufahamisha kuwa Naomi alifariki dunia.

Hata hivyo kesho mchana Mahakama hiyo inatarajia kusoma hukumu dhidi ya mshtakiwa huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Vyema,kesi hii imesikilizwa vyema japo sio kwa haraka kama zingine. Mf,Kesi ya Respicius Mutazangira

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...