Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii
MAFUNZO ya lugha ya programu za (programming Language), yanayotolewa kwa wataalamu wa hali ya hewa kutoka vituo mbalimbali vya hali ya hewa nchini, yatakuwa na manufaa makubwa katika sekta hiyo ya hali ya hewa na kuongeza usahihi wa utabiri wa hali ya hewa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo,  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Dkt. Agnes Kijazi amesema kupitia mafunzo hayo anatarajia kuona ongezeko la ujuzi wa wachambuzi wa data za hali ya hewa na watakaopelekea kuongezeka kwa usahihi wa utabiri wa hali ya hewa.

Mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika katika Ukumbi wa wa Mikutano, Tari Kibaha,  yameandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Norway na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kupitia Awamu ya Pili ya programu ya Kidunia ya Utoaji wa Huduma za Hali ya Hewa ya GFCS (Global Framework for Climate Services Adaptation Programme in Africa (AP).

"Ni mategemeo yangu kuwa, matokeo ya jumla ya mafunzo haya yataleta mabadiliko katika Mamlaka ikiwa ni ongezeko la jumla la usahihi wa taarifa zinazotolewa na ongezeko la ujuzi wa wafanyakazi katika uchambuzi wa data za hali ya hewa", Amesisitiza Dkt. Kijazi.
Ameeleza kuwa, akiwa kama mmoja wa wajumbe kumi wanaomshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) katika masuala ya teknolojia anatambua kuwa teknolojia ni jambo muhimu sana ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu na hivyo kupitia mafunzo hayo anawataka washiriki kujikita katika kufikia malengo hayo katika utoaji wa huduma wa za hali ya hewa.

Kwa upande wake, mratibu wa mafunzo hayo na mtaalamu wa hali ya hewa mwandamizi Dkt. Habiba Mtongori amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea wataalamu wa hali ya hewa maarifa ya msingi katika lugha ya programu za kisayansi (CDO na R) ambazo zitawajengea uwezo wa kushughulikia idadi kubwa ya data za hali ya hewa  kwa muda mfupi na kuchakata takwimu mbali mbali kutoka katika data hizo ili kutoa huduma bora na za uhakika zitakazotumiwà na wadau mbalimbali wa TMA.

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo Bi. Asya kutoka kituo cha Zanzibar amesema, mafunzo hayo yatamuongezea ufanisi wa kazi zak kwa manufaa ya Mamlaka na Taifa kwa ujumla kupitia huduma za hali ya hewa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...