Na Khadija seif, Michuzi TV
MSANII Mkongwe wa bongofleva nchini Abas akili alimaarufu Abbyskills amefurahishwa na kujivunia uwepo wa Ali kiba na Nasibu Abdul (Diamond platinum) katika Muziki wa bongo fleva kwa Sasa.

Abbyskills amesema akiwa kama Kaka na mkongwe kwenye fani hiyo anajivunia Sana kuona vijana hao wawili wakileta mapinduzi kwenye Muziki na kupelekea nchi ya Tanzania kutambulika sehemu mbalimbali kwa urahisi kupitia Sanaa ya Muziki.

" Zamani kulikua na ugumu kiasi hasa linapokuja swala la kujitambulisha tunapokua nchi za wenzetu na kielelezo kilikua kimoja tu kuwa natokea nchi ya Tanzania yenye mlima Kilimanjaro lakini kwa Sasa Kuna wepesi sana wanajua kabisa natokea nchi ya msanii Alikiba pamoja na Diamond platinum na imekua rahisi hata hao wenzetu kutaja baadhi ya nyimbo wanazozipenda kutoka kwa wawili hao".

Mbali na hilo Abbyskills ameeleza kuwa kwa sasa Diamond platinum anamfananisha na Mr.nice huku Alikiba akifananishwa na Mr.blue.

"Kutokana na utunzi wake platinum ambao akitoa nyimbo basi haitochagua rika maalumu huku akitaja yope kuwa ni mfano hai ,na kwa upande wa kiba kuwa kama Mr.blue kwa sababu anatengeneza muziki unaoishi ambao wote kwa pamoja wanaotoa burudani nzuri na Muziki wao unawateka watu wote".

Aidha amewatoa hofu mashabiki wake kuwa uhusiano waliojenga yeye na Alikiba bado upo na hawana ugomvi wowote licha ya watu wa mitandaoni kutafsiri hivyo kutokana na kutochaguliwa kuwepo kwenye tour iliyoifanya Desemba mwaka Jana katika Mkoa wa Tabora na Iringa.

"Kama sikuitwa mikoa hiyo tutegemee nitaitwa mikoa inayofata niwatoe hofu kwenye hilo Kings Muziki ni ndugu zangu, jamaa zangu na wakati linaanzishwa nilikuwepo pia na Alikiba ni mdogo wangu tumetoka mbali sana na nimefanya nae kazi mbalimbali na zilizofanya vizuri miaka hiyo kama wimbo wa Maria,"

Pia amewaomba mashabiki wote wanaopenda muziki mzuri kuipokea kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la herena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...