Naibu Rais wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Bw. James Gitau, akiwa katika
mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge. Mazungumzo
yaliyofanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge
akimfafanulia Naibu Rais wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia
watoto (UNICEF) Bw. James Gitau wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo
katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Comoro nchini Tanzania
Mhe. Balozi Ahamada Elbadaour Mohamed akiongea na Mkuu wa Itifaki wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali
Wilbert Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika 22 Januari 2020 katika
Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge
akimfafanulia jambo Balozi wa Comoro nchini Tanzania Mhe. Balozi Ahamada
Elbadaour Mohamed wakati wa mazungumzo yaliyofanyika 22 Januari 2020
katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe.
Balozi Frederic Clavie akiongea na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge
wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge
akimfafanulia jambo Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Balozi Frederic
Clavie wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge
akiongea na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Aga Khan (AKDN)
Bw. Amin Kurji.
Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe.
Balozi Yonas Yosef Sanbe akiongea na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibugea
kiongea na Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe. Balozi Yonas Yosef Sanbe
Balozi wa Iran nchini, Mhe. Balozi
Mousa Farhang akimsikiliza Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati
walipokutana kwa ajili ya mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Denmark nchini Mhe.
Balozi Mette Norgaard akimsikiliza Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge
wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Italia nchini Meh.
Balozi Roberto Mengoni akimsikiliza Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge
wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
……………
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A.
Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi mbalimbali
wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Wakuu wa Mashirika ya
Kimataifa tarehe 22 na 23 Januari 2020 katika Ofisi ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalilenga
kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi hizo na
mashirika hayo.
Mabalozi hao ni Balozi wa
Visiwa vya Comoro, Mhe. Balozi Ahamada Elbadaour Mohamed, Balozi wa
Ufaransa nchini, Mhe. Balozi Frederic Clavie, Balozi wa Denmark nchini
Mhe. Balozi Mette Norgaard na Balozi wa Iran nchini, Mhe. Balozi Mousa
Farhang, Balozi wa Ethipia nchini, Mhe. Balozi Yonas Yosef Sanbe, pamoja
na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Balozi Roberto Mengoni.
Mbali na mabalozi, Mkuu wa
Itifaki, Balozi Kanali Ibuge amekutana na Wakuu wa Mashirika ya
Kimataifa ambao ni Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la kuhudumia watoto (UNICEF) Bw. James Gitau na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Aga Khan (AKDN) Bw. Amin Kurji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...