Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) mkoani Singida jana.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Pascas Muragiri akizungumza mda mfupi kabla ya kumkaribisha Waziri Dkt. Harison Mwakyembe kuzungumza na wanahabari. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini TBC, Ayoub Ryoba, akiwaeleza waandishi wa habari mkoani Singida (hawapo pichani)dhima hasa ya chombo hicho cha taifa, na namna hatua kwa hatua wanavyoendelea kwa kasi kuboresha huduma za shirika hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) 
Wanahabari na Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Singida wakifatilia. 
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Singida, Seif Takaza, akizungumza kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Kaimu Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Singida, Bibie Mssumi akizungumza na waandishi wa habari juu ya madhara ya Rushwa katika uchaguzi.
Mwandishi wa Standard Radio mkoa wa Singida, Festo Sanga akichangia.
Na Godwin Myovela, Singida
WAZIRI waHabari, Utamaduni, Sanaa naMichezo, Dkt. Harison Mwakyembe amesema sheria tarajiwa ya habari inakwenda kuleta mageuzi makubwa kwa kuipa hadhi tasnia nzima ya uandishi wa habari,ikiwemo kuifanya ianze rasmi kutambulika kama zilivyo taaluma zingine, huku akisisitiza hakuna yeyote mwenye kiwango cha elimu ya tasnia hiyo chini ya stashahada, atakaye ruhusiwa kujishughulisha na uandishi wa habari baada ya 2021.
Mwaka 2016 serikali ilitoa muda wa miaka mitano kwa wanahabari wote wasio nasifa ya kiwango cha elimu kuanzia ngazi ya Diploma nakuendelea kuhakikisha wanajiendeleza kufikia hatua hiyo,na kwamba ifikapo mwaka kesho ndio utakuwa ukomo wa mudastahiki.
Mwakyembe aliyasema hayo kwenye kikao chake na wanachama wa chama cha Wanahabari mkoani hapa,‘Singida Press Club’wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua hali ya usikivu kwa wananchi kupitia Radio naTelevisheniyaTaifa TBC1 na TBC Fm.
“Na kuhususuala la elimu hatutarudi nyuma, tunajua wanahabari wengi watapoteza hii kazi, ila umuhim wa haya tunayo ya chukua sasa hapo baadaye yatanyanyua sana hadhi na kuipa heshima taalumahii…nani wahakikishie kama mtu anadhani serikali itatetereka kuhusu hili afute hiyo kichwani, ‘it’s not our concerns,’” alisemaMwakyembe.
Akizungumza kuhusu tija na mageuzi ya takayo tokana na uwepo wa sheria hiyo ya habari, alisema kwanza inakwenda kuanza kuitambulisha rasmi taaluma ya uandishi wa habari, sanjari na kutoa mamlaka ya kuundwa kwa bodi ya‘ithibati’, 
chombo ambacho kitaainisha na kutambua nani anastahili kuwa mwana-taaluma na nani amekosa sifa kisheria.Aidha, Mwakyembe alisema, sheria hiyo ina kwenda kuunda Baraza Huru la Habari, baraza ambalo litaundwa na wanahabari wenyewe, ambao tayari watakuwa wamepitia kwenye ithibati na kuthibitika kisheria pasiposhaka kuwa haoni wanahabari.
Alisema, pia sheria hiyo inaunda Kamati ya Malalamiko, ambayo imepewa madaraka chini ya sheria ya kimahakama ambapo mwenyekiti akiamua jambo lolote kwenye hiyo kamati maamuzi yake ni sawa na maamuzi ya Hakimu waWilaya au HakimuMkazi.
Hata hivyo, Waziri huyo wa Habari aliweka wazi kwamba kutokana na taaluma hiyo kuwa adhimuna kwa kuzingatia ndiyo yenye jukumu la kutoa elimu na taarifa mbalimbali kwa wananchi kupitia sheria hiyotarajiwa kutakuwa na Mfuko wa Elimu kwa wanahabari,sambamba na kuhakikisha kila mwana-taaluma anakuwa nabima.
“Tasnia hii inahitaji vijana wenye upeo mpana, waadilifu, wenye weledinanidhamu. Na hii sheria itatufikisha huko….kwa hiyo lengo letu kubwa tukishaunda vyombo vyote hivyo tuwe natasnia ya habari inayojiendesha yenyewe,” alisemaMwakyembe.
Ili kuletatija na ubora wa kiutendaji, na kwakuzingatia matakwa ya kisheriaifikapo 2021, serikali imewahakikishia wanahabari kuwa itaangalia namna bora ya kujadiliana kwa pamoja juu ya uboreshaji wa maslah ina stahiki nyingine, kwa kuanzia na kiwango cha kima cha chini cha mshahara
“Pia tunakusudia kukaa chini kuaininisha na kuoanisha mitaala ya ufundishaji wa wanahabari, ili kwenda sambamba na matakwa na ubora stahiki, nasio kila mtu kuibuka na kuanzisha chuo chake cha uandishi wa habari na kufundisha anachokijua yeye hapana! hiyohaikubaliki,” alisemaWaziri
Akifafanua kuhusu azma chanya kisheria kuhusu haki ya kupata habari au taarifa na huduma ya habari, alisema lengo lake nikuzidi kuboresha ile ibaraya 18(d) katika kumsaidia mwananchi kupata taarifa kwa njiambalimbali. Na chini ya sheria hiyo na kanuni zake kila mamlaka ina msemaji
“Badala ya kutafuta taarifa vichochoroni au kwenye vyanzo visivyosahihi nenda kwa mtu sahihi iliakupe taarifa zisizo za upotoshaji,”
Katika hatua nyingine, akizungumzia kuhusu uchaguzi mkuu ujao, Mwakyembe alisema serikali haitavumilia na kwamba itachukua hatua kali sana kwa chombo chochote au mwandishi yeyote wa habari atakaye jaribu kufanya upotoshaji wakati wa mchakato mzima wauchaguzi huo.
Alisemakipindi cha uchaguzi ni kipindi ambacho kama watanzania tunapaswa kuonyesha mshikamano wa kitaifa, lakini kwa wanahabari suala la maadili, sanjari na kuheshimu sheria, kanuni na taratibu huku akiwataka kutumia kalamu zao vizuri ili kuepusha madhara ya uvunjifu wa amani, ambayo yanaweza kulipeleka taifa kwenye matatizo makubwa.
“Na katika hili kwa kweli tutakuwa wakali sana, nasubiri tume ya uchaguzi itawaita wanahabari wote…na safari hii naomba ni wahakikishie hata watua mbao wapokwenye mitandao ya kijamii kupitia ‘online Tvna online Radio’ kwa mba na wao watafata sheria zote za wanahabari vinginevyo tutasimamisha leseni zao,” alisema na kuongeza:
“Nawasihi sana wanahabari nyakati za uchaguzi muda ukifika tusitumike kuchafuana, tusirubuniwe na pesa navibahasha…tuache kuandika habari kwa kigezo cha fedha tusimamie misingi na maadili.”
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani hapa, Seif Takaza, kuhusu suala la kujiendeleza alimwomba Waziri kuangalia namna ya kuwasaidia wanahabari hao kupitia fungu lolote maalumu huku akisisitiza kuwa wanapenda kujiendeleza kielimu kulingana naagizo la serikali lakini kipato chao hakitoshelezi.
AidhaTakaza alisema suala linalowasumbua zaidi waandishi wa mkoa huo nikitendo cha kufanya kazi bila ya kuwa na mkataba wowote wa mwajiri, ikiwemo ulewa hali bora, hukustahiki zikiwa ni ndogo sana hali inayopelekea wao kujiingiza kwenye shughuli nyingine iliangalau kukidhi mahitaji.
“Tunaamini watanzania na hata nje ya taifa letu wanampenda sana Rais John Magufuli kupitia vyombo vya habari…kwa kweli asiye mpenda labda ni mchawi, tunaomba serikali iangalie namna nzuri ya kuboresha na kutatua changamoto zinazo tukabili ikiwepo kutupatia viwanja vya kujenga Clubs zetu kuliko kupanga kama ilivyosasa,” alisemaTakaza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...