Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
UTAFITI uliofanywa na Taasisi ya HakiElimu nchini umeonyesha kuwa ushiriki hafifu wa wazazi au walezi katika kuhamasisha watoto kufanya vizuri mashuleni na uhusiano mbaya na walimu ni moja ya chanzo cha watoto wengi kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya Kitaifa kwa mfululizo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ripoti ya utafiti wa sababu zinazochangia baadhi ya mikoa kufanya vizuri huku mikoa mingine ikifanya vibaya mfululizo katika mitihani ya darasa la saba Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage amesema, utafiti huo uliofanywa ukiwa na lengo la kubaini sababu zinazosababisha baadhi ya mikoa kufanya vibaya na mingine kufanya vizuri.

Amesema, katika utafiti huo uliofanywa kwa kipindi cha miaka miwili, 2018 hadi 2019 umebaini sababu mbali mbali za baadhi ya mikoa kufanya vibaya mfululizo kuwa ni  nafasi hafifu ya wazazi na walezi katika kuhamasisha watoto kufanya vizuri kwenye masomo na mitihani yao ya mwisho, umbali mrefu kutoka nyumbani kwenda shuleni na kutoka shuleni kwenda makao makuu ya wilaya.

Aidha amezitaja sababu zingine kuwa ni tofauti ya kimiundombinu ama mazingira kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, kutokuwapatia motisha ama hamasa walimu na mbinu za ziada ili kuimarisha ufundishaji na kujifunza pamoja na kuwapo kwa changamoto katika masuala ya kimenejimenti.

Dk. Kalage ameitaja baadhi ya mikoa iliyoonekana kufanya vibaya katika kipindi cha miaka mitano kuwa ni Singida, Dodoma, Mtwara, Mara,Tanga,Kigoma, Tabora na Manyara.

Aidha baadhi ya mikoa inayoonekana kufanya vizuri ni pa moja na Arusha Dar es Salaam, Geita, Iringa, Kilimanjaro na Kagera na kubainisha kuwa sababu mojawapo inayofanya mikoa hiyo kufanya vizuri ni kuwepo na ubora wa kiutawala na Kimenejimenti katika ngazi ya shule na Wilaya, mbinu za ziada kuimarisha kufundisha na kujifunza katika ngazi za mkoa na wilaya na ushiriki wa wazazi na uhusiano mzuri baina yao na walimu na motisha kwa walimu.

Katika utafiti huu, HakiElimu kwa kutumia ripoti ya matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la saba 2016 na 2017 tumechagua mikoa michache iliyofanya vizuri pamoja na michache iliyofa vibaya kwa minajili ya kujifunza ma kubaini matokeo yao ili iwe chachu kwa mikoa mingine kujitathmini na kutafuta sababu zinazopelekea ama ufanye vizuri, wastani au vibaya" amesema Dk. Kalage. 

Amesema, anaamini kuwa utafiti huo utaongeza tija kwa mikoa ambayo ilikuwa inafanya vibaya kwa kujifunza kutoka mikoa inayofanya vizuri na kupelekea kila mkoa kufanya vizuri ili kuwa na uhakika wa kuwa na watoto wengi zaidi watakaopata fursa ya ufaulu na kuendelea na masomo.

"Ni matumaini yangu kwamba matokeo ya utafiti huu yatachochea mijadala kuhusiana na matokeo ya ujifunzaji kwa watoto wetu na namna bora ya kuboresha ufaulu ili kuinua elimu yetu.

Kwa upande wake, Mashauri Mkuu wa utafiti huo, Dk. Richard Shukia amesema walikwenda katika mikoa 10 wakati wa kufanya utafiti na kuongeza kuwa matokeo ya utafiti huo yatachangia kuongeza ufaulu katika baadhi ya mikoahasa ile iliyofanya vibaya.

 Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu,  Dk.John Kalage akizungumza na Waandishi  wa habari wakati wa uzinduzi  wa ripoti ya utafiti  uliofanywa na kuangazia baadhi ya mikoa inayofanya vibaya kila mwaka na mingine kufanya vizuri.
 Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu,  Dk.John Kalage akikata utepe kuonyesha uzinduzi wa ripoti ya utafiti  uliofanywa na kuangazia baadhi ya mikoa inayofanya vibaya kila mwaka na mingine kufanya vizuri. Kushoto kwake ni aliyeshika ripoti ni Mkuu wa Miradi HakiElimu, Boniventure Godfrey kulia anayeangalia ni meneja Idara ya Habari, Elisante Kitulo na mwisho kushoto ni Robert  Mihayo, mdhibiti ubora HakiElimu.
 Baadhi wa waandishi wa habari na wadau wa HakiElimu wakifuatilia ripoti ya utafiti uliofanywa na kuangazia baadhi ya mikoa inayofanya vibaya n mingine kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya Kitaifa kwa ngazi ya elimu ya msingi.
 Baadhi ya ripoti zikioneshwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...