Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
IMEELEZWA
kuwa Marekani imeongeza nchi saba zaidi zinatarajiwa kuongezwa katika
orodha ya nchi ambazo zimezuiliwa kuingia nchini humo na kuelezwa kuwa
nchi hizo zitazuiwa kupata baadhi ya Visa pamoja na kutolewa katika
ushiriki wa bahati nasibu ya green card, vyombo vya habari vya Marekani
vimeripoti.
Imeelezwa
kuwa Rais wa Marekani Donald Trump akiwa David nchini Uswizi kupitia
gazeti la Wall Street Journal amethibitisha mpango wake kuongeza idadi
ya nchi katika orodha ya nchi zilizozuiwa kuingia nchini humo.
Imeelezwa
kuwa nchi ambazo zinaweza kuwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Myanmar,
Nigeria, Sudan, Tanzania, Eritrea, Belarus na Kygyzstan.
Ikumbukwe
kuwa mwaka 2017 Trump akisaini zuio la namna hiyo kwa nchi zenye
waislamu wengi zaidi ikiwemo Iran, Iraq, Syria, Yemen, Libya, Somalia,
Venezuela, Korea kaskazini na Chad ambayo iliondolewa mwaka 2018.
Orodha
ya nchi hizo zinategemewa kuchapishwa mapema Januari 27 huku shirika la
habari la Kimataifa la Reuters limeripoti kuwa mmoja wa Mwandamizi wa
Serikali ya Rais Trump amedokeza kuwa orodha hiyo inakuja baada nchi
hizo kushindwa kufuata masharti ya kiusalama ikiwemo taarifa za alama za
vidole pamoja na taarifa za mapambano ya kigaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...