BENKI ya Ecobank Tanzania wameanzisha rasmi programu ya kufanya kazi pamoja na wahitimu wa vyuo vikuu kwa kushirikiana na benki hiyo kwa muda wa mwaka mmoja ili kuwapatia uzoefu wa kazi na kuwaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank Mwanahiba Mzee amesema kuwa wameanzisha kampeni hiyo ambayo wanafunzi kumi waliomaliza vyuo mwaka jana na juzi wanaungana na  benki hiyo kwa mwaka mmoja kwa ajili ya mafunzo ya kazi ili kuwatayarisha kuwa mameneja na wakuu wa vitengo wajao.

Amesema kuwa moja ya majukumu ya benki hiyo ni kuendeleza na kushiriki katika katika sekta ya elimu nchini na wamekuwa wakishirikiana na ukaribu  na Serikali, shule na vyuo mbalimbali ikiwemo chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na chuo Cha usimamizi wa fedha (IFM) ambavyo vimekuwa vikitoa wanafunzi wa kujitolea katika benki hiyo.

Mwanaiba amesema kuwa wameshirikiana na vyuo vya UDSM na IFM ili kupata wanafunzi bora na kufanya nao kazi  na kueleza kuwa uhusiano huo ni wa muda mrefu ambao umeanza kuzaa matunda.

" Wahitimu 120 waliomba nafasi hizo na 90 waliingia katika usahili wa mahojiano na kumi ndio waliochaguliwa na wale ambao walipita katika nafasi hiyo watapewa kipaumbele fursa zikitokea" amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa shahada za juu Dkt. Diana Mwiru ameeleza kufurahishwa na jambo hilo ambalo benki hiyo imelichukua na kusema kuwa wahitimu wengi wamekuwa wakikupambana na changamoto ya kutokuwa na uzoefu pindi wanapoomba nafasi za kazi.

Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yanayotolewa na benki hiyo yatawasaidia wahitimu hao kuhamisha nadharia walizozipata darasani kwa kujifunza kwa vitendo.

Dkt. Mwiru amesema kuwa benki hiyo inawasaidia pia katika mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi kila mwaka na kuzishauri taasisi za namna hiyo kuwa na programu za namna hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ,Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanzishwa rasmi kwa programu ya kufanya kazi pamoja na wahitimu wa vyuo vikuu kwa kushirikiana na Benki ua Ecobank leo katika ofisi zake zilizopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Shahada na Shahada za Juu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Diana Mwiru akizungumzia mchakato unaofanyika chuoni hapo wanapokuwa wanawatafuta wanafunzi bora ili waweze kujiunga na programu ya kufanya kazi na Ecobank kwa mwaka mmoja  ili wanafunzi hao waweze kupata uzoefu katika kazi zao.
Mkurugenzi wa Shahada za Awali kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dkt. Shaban Ngole akitoa shukrani kwa Ecobank kuweza kuchukua wahitimu kutoka kwenye vyuo kwa takribani mwaka mmoja ili kiwapa uziefu wa kazi na kuwaandaa kiwa viongozi bora wa baadae

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...