Na. Aaron Mrikaria - Rungwe
Watendaji wa Halmashauri zinazonufaika na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) watakiwa kubeba dhamana ya kutoa elimu kuhusu manufaa ya hatimiliki za kimila ili walengwa wa mpango huo wanufaike kupitia hati hizo.

Wito huo umetolewa jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kwa Watendaji wa Halmashauri akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Rungwe yenye lengo la kukagua  utekelezaji wa miradi ya MKURABITA.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema nimetembelea miradi ya MKURABITA iliyopo katika baadhi ya Halmashauri na kugundua kuwa Watendaji wa Halmashauri ilipo miradi hiyo hawatekelezi wajibu wao wa kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kurasimisha raslimali na biashara zao.

“Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri hakikisheni katika mpangokazi wenu mnaliwekea kipaumbele suala la elimu kuhusu MKURABITA kwa sababu lina manufaa kwa wananchi ambao Mhe. Rais, Dtk. John Pombe Magufuli amekuwa mstari wa mbele kuwawezesha”. 

Aidha, Dkt. Mwanjelwa amezishukuru baadhi ya taasisi za kifedha kwa kutambua Hatimiliki za Kimila na kutoa mikopo ya zaidi ya shilingi milioni mia tisa kwa wakulima wa chai wa Wilaya hiyo, ikiwemo Benki ya CRDB, NMB na SACCOS ya kijiji cha Ntandabala.

Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Serafia Mgembe amesema wananchi waliopata hatimiliki za kimila wanakabiliwa na changamoto ya kutokujua namna ya kuzitumia hati hizo kupata mikopo ikiwemo ujuzi wa kubuni miradi na namna ya kuandika mpangokazi wa  kuombea mkopo.

Dkt. Mgembe amezishauri taasisi za kifedha zifungue dirisha la kutoa elimu kwa wananchi ili iwe rahisi kwao kutambua namna wanavyoweza kupata mitaji na kujiendeleza kiuchumi.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) yuko mkoani Mbeya katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji  wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).

 Naibu Waziri  Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na  wanakijiji wa Ntandabala kata ya Masoko Wilayani RUNGWE katika ziara ya kikazi ya kukagua mradi wa kurasimisha raslimali za wanyonge ( MKURABITA).
 Baadhi ya Wazee na Vijana wa kijiji cha Ntandabala kilichopo Kata ya Masoko Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wakimsikiliza, Naibu Waziri  Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa  alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya uamuzi wa serikali kuanzisha mpango wa kurasimisha raslimali za wanyonge (MKURABITA) na faida zake kwa wanufaika.

Baadhi ya akina Mama wa Kijiji cha Ntandabala kilichopo kata ya Masoko Wilayani Rungwe wakimshukuru  Naibu Waziri  Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa kwa kufanya ziara kijijini hapo na kutoa  maelekezo yatakayowasaidia kutatuliwa kero zao za kurasimishiwa maeneo yao na kunufaika na mikopo katika taasisi za fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...