WATANZANIA  wameshauriwa kuchangamkia fursa  katika vyuo vya elimu ya juu nje ya nchi  ili kupata ujuzi  unaoendana na  mabadiliko ya haraka ya teknolojia.

Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na  Mwambata wa Mwenza  wa Taasisi ya Elimu ya Juu ya Edugate  ya Uingereza  Aliyuthuman  Sadhique  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi  wa programu  maalumu ya kusaidia wanafunzi  katika nchi zenye uchumi wa kati  inayofahamika kama LICAP.

Amesema program hiyo  inalenga kuwafikia  wanafunzi na wahitimu  mbalimbali  kutimiza malengo  katika vyuo maalumu vilivyopo Uingereza na Sri Lanka.“Edugate  kwa kushirikiana na  Taasisi ya  British Colledge  of Upplies  Studies ya Sri Lanka tumedhamilia kuwekeza  katika elimu hapa nchini hususan kuwawezesha watanzania kwenda kusoma nje  ya nchi ikiwemo kuwasaidia  kimasomo,”amesema.

Ameongeza kuwa "Leo tutazindua  program hiyo ambapo uzinduzi  utaaendana na  kongamano  maalumu litakalo toa fursa  kwa watanzania kuzitambua fursa hizo za elimu,"Sadhique amesema kongamano  halitakuwa na  malipo yoyote  na mtu yoyote anaweza kuhudhuria  hususan wenye nia ya dhati ya kwenda kujiendeleza nje ya nchi.

Amewataka wale wote wenye nia ya kusoma  nje ya nchi kuhudhuria  kongamano hilo na kwamba litakuwa na faida kubwa  husan kwa wahitimu wa Teknolojia ya habari na Mawasiliano (IT), Usimamizi wa fedha, uhandisi  na taaluma zingine .

Amesema kwamba kwa wale ambao ufaulu wao utaonekana kuwa ni wajuu  watasaidiwa kupata  udhamini  kupitia program hiyo  ya  LICAP.

Mmoja wa waratibu wa kongamano hilo David Munanka, amesema  mafunzo hayo  yamekuja wakati muafaka ambapo serikali ya awamu ya tano inatekeleza dira yake ya kuelekea uchumi wa viwanda na kuongeza mwenye sifa  na nia ya kusoma shahada au astahashada nje ya nchi anaweza kuhudhuria kongamano hilo bure.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...