Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
IRAN
imekiri kuidungua kimakosa ndege ya abiria ya Ukraine (Boeing 737) na
kuua abiria wote 176 waliokuwamo na kueleza kuwa makosa ya kibinadamu
yalitokea baada ya ndege hiyo kukatisha katika eneo linalomilikiwa na
kikosi cha Mapinduzi cha nchi hiyo na kueleza kuwa maafisa waliofanya
kosa hilo watachukuliwa hatua.
Televisheni
ya taifa ya Iran imetoa taarifa hiyo leo ambapo awali Iran ilikanusha
kutohusika na udunguaji wa ndege hiyo katika Mji kuu Terhan siku ya
Jumatano.
Pia taarifa
hiyo imefuatiwa na radhi iliyoombwa na Rais wa Iran Hassan Rouhani
ambaye ameeleza kuwa Serikali inajutia kitendo hicho kilicholeta madhara
makubwa na kuelekeza maombi na sala zake kwa wafiwa na familia
zilizoathirika.
Pia
Waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo Javad Zarif ameomba radhi kwa
familia, wafiwa na mataifa yaliyoathirika na tukio hilo na kusema kuwa
ndege hiyo ilidunguliwa kwa bahati mbaya baada ya kupitia sehemu nyeti
ya jeshi.
Hii inakuja siku chache baada ya Iran kukana madai ya wachunguzi kutoka nje ambao waliinyooshea kidole nchi hiyo kwa kuhusika
na
tukio hilo ambalo mara baada ya kutokea Rais wa Marekani Donald Trump
alieleza akuwa Iran inahusika na shambulio hilo huku Waziri Mkuu wa
Canada Justin Trudeau akisema kuwa vyombo vya usalama vya Canada vina
ushahidi kuwa Iran imeitungua Boeing 737.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...