Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu (Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko, akisisitiza
umuhimu wa kutekeleza majukumu ya Ofisi hiyo kwa Ufanisi wakati
alipokutana na maafisa wa Ofisi hiyo, ikiwa ni utaratibu aliouanza wa
kukutana na watumishi wa ofisi hiyo leo, tarehe 16 Februari, 2020,
Jijini Dodoma
Baadhi ya maafisa
wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa
mkutano na maafisa hao, ikiwa ni utaratibu aliouanza wa kukutana na
watumishi wa ofisi hiyo leo, tarehe 16 Februari, 2020, Jijini Dodoma.
Ofisa kutoka
Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Edgar Senga,
akiongea katika kikao cha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu na
Uwekezaji), Dorothy Mwaluko, (hayupo pichani) wakati wa mkutano na
maafisa hao, ikiwa na utaratibu aliouanza wa kukutana na watumishi wa
ofisi hiyo leo, tarehe 16 Februari, 2020, Jijini Dodoma.
Ofisa kutoka
Idara ya Bunge na Siasa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ernajoyce Hallo, akiongea
katika kikao cha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu na
Uwekezaji), Dorothy Mwaluko, (hayupo pichani) wakati wa mkutano na
maafisa hao, ikiwa na utaratibu aliouanza wa kukutana na watumishi wa
ofisi hiyo leo, tarehe 16 Februari, 2020, Jijini Dodoma.
Baadhi ya maafisa
wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa
mkutano na maafisa hao, ikiwa ni utaratibu aliouanza wa kukutana na
watumishi wa ofisi hiyo leo, tarehe 16 Februari, 2020, Jijini Dodoma.
********************************
Kwa mujibu wa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, Ibara 52,
jukumu la msingi la Ofisi ya Waziri Mkuu ni kuratibu na kusimamia
shughuli za Serikali katika sekta zote na Bungeni, Aidha Tangazo la
Serikali Na. 144 Aprili 2016, lililofanyiwa mabadiliko tarehe 7 Oktoba
2017, limeaninsha majukumu mengine yanayosimamiwa na kuratibiwa na Ofisi
hiyo.
Katika
kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Ofisi hiyo
yanaboreshwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu na Uwekezaji),
Dorothy Mwaluko, ameamua kukutana na watumishi wa Ofisi hiyo katika
makundi ya Maafisa, Watumishi wasio maafisa na Wakurugenzi kwa nyakati
tofauti, ambapo leo tarehe 16 Februari 2020, ameanza kukutana na
maafisa wote wa ofisi hiyo, Jijini Dodoma.
Akiongea na
maafisa hao amewataka kuzingatia taratibu, sheria na kanuni za utumishi
wa umma katika kuratibu na kusimamia shughuli za serikali. Aidha,
amebainisha kuwa katika kuhakiksha utekelezaji unakuwa wa ufanisi
ataandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa hao ili kuboresha utendaji
kazi wao.
“Maafisa ndio
watu wanaoanza kuchakata shughuli nyingi za utekelezaji, Taarifa za
uratibu wa shughuli za serikali zikiandaliwa vizuri kabla ya kumfikia
mkurugenzi matokeo yake huwa ni mazuri. Niwasihi jitumeni na ongezeni
umakini katika kutekeleza majukumu, pia shirikishaneni, ili muweze
kufanikiwa kutekeleza vyema jukumu la msingi la ofisi hii” Amesisitiza,
Katibu Mkuu, Mwaluko.
Aidha,Katibu Mkuu
mwaluko amesisitiza ushirikiano katika utendaji wa majukumu usizingatie
kada tu, au maafisa ndani ya Idara na vitengo bali ushirikiano pia uwe
kati ya Idara na vitengo, lengo ni kuhakikisha kila afisa anakuwa na
uwezo wa kumudu kuratibu na kusimamia shughuli za serikali kwa ufanisi.
Majukumu ya
msingi yanayosimamiwa kwa sasa na Ofisi hiyo ni:- Uratibu wa Shughuli
za Serikali; Kuongoza Shughuli za Serikali Bungeni; Kuratibu
Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa; Usimamizi na Uratibu wa Shughuli za
Dharura na Maafa.
Aidha Ofisi hiyo
ndiyo inaratibu, Shughuli za Uwezeshaji wananchi kiuchumi, na Maendeleo
ya Sekta Binafsi, shughuli za Kuwezesha Maendeleo ya Uwekezaji na
shughuli za Kuboresha mazingira ya Biashara nchini.
Shuguli nyingine
zinazoratibiwa na kusimamiwa na ofisi hiyo ni Mapambano dhidi ya janga
la UKMIWI na usimamizi wa athari zake kwa Tanzania Bara, Mapambano
dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya , Shughuli za Uchaguzi
nchini, Masuala ya Vyama vya Siasa na Ofisi hiyo ndiyo inayochapa
rasmi nyaraka za Serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...