Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Arusha David Lyamongi wakati akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa vyombo vya habari nchini
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha Cloud Gwandu akizungumza katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kufanyika katika ukumbi uliopo ofisi ya mkuu wa mkoa Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) Joseph Butiku aliwataka waandishi wa habari nchini kujiuliza na kujitazama juu ya tahamani ya Taifa
Mwandishi wa Habari kutoka kituo cha ITV akiwa katika warsha hiyo.
Waandishi waliojitokeza kwaajili ya warsha ya siku moja wakiwa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa moa Arusha
Baadhi ya waandishi wa habari waliohidhuria warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ikiwa na lengo la yenye lengo la kulinda na kudumisha amani kipindi cha uchaguzi mkuu
Baadhi ya waandishi wa habari waliohidhuria warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ikiwa na lengo la yenye lengo la kulinda na kudumisha amani kipindi cha uchaguzi mkuu
Baadhi ya waandishi wa habari waliohidhuria warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ikiwa na lengo la yenye lengo la kulinda na kudumisha amani kipindi cha uchaguzi mkuu
Na.Vero
Ignatus,Arusha
Wadau wa
habari nchini wameaswa kutumia kalamu zao kwa weledi uzalendo na utaifa kama
nyenzo za uandishi wa habari kwa lengo la kuhakikisha suala zima la Amani ya nchi
linapewa kipaumbele wakati wote wa kabla na baada ya uchaguzi mkuu ili kulinda
Amani na Umoja wa Taifa.
Kauli hiyo
imetolewa na Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Arusha David Lyamongi wakati
akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa vyombo vya habari nchini yenye lengo
la kulinda na kudumisha amani kipindi cha uchaguzi mkuu iliyoandaliwa na
taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF)
Alisema kuwa
bila vyombo vya habari hakuna jambo lolote litakalofanikiwa kwani ni muhimili wan
ne baada ya mihimili mitatu ya kikatiba hivyo busara inahitaji ikiendana na
maadili ya uandishi wenye weledi na uzalendo kwa taifa lao.
Akaeleza
kuwa sehemu yoyote duniani vyombo vya habari ni muhimu katika kuhabarisha umma
kwenye suala zima la maendeleo hivyo kama hawatakuwa na weledi na utaifa
wanaweza kuipelekea na kutumia vibaya tasnia hiyo hivyo nchi kujikuta ikiingia
katika mchafuko.
’’Niwaombe
waandishi wa habari nchini kuweka mbele utaifa weledi uzalendo katika
kutekeleza majulumu yenu wakati wote tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu kwa
kutumia kalamu zenu vizuri katika kujenga na kudumisha amani ,umoja ,maendeleo
na mshikamano wakati wote kabla na baada ya uchaguzi mkuu’’
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) Joseph Butiku
aliwataka waandishi wa habari nchini kujiuliza na kujitazama juu ya thamani ya
Taifa lao katika kuhakikisha umoja ,maadili na mshikamano vinaendelea
kudumishwa wakati wote wa uchaguzi mkuu pamoja na maisha ya kila siku ili
kuleta maendeleo
Akawasihi
kuhakikisha wanaimarisha mshikamano uliyopo nchini kwa kutumia taaluma yao
katika kuhakikisha Taifa linaendelea kudumisha Amani ,mshikamano uzalendo na
Utaifa kwa kujenga weledi wa taarifa zao wanazoziandika katika kukuza maendeleo
ya Taifa.
‘’Kazi
kubwa ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) ni kuhakikusha kuwa kukuza na
kuimarisha uwezo wa viongozi na wananchi kwenye maswala ya uchaguzi,amani,umoja
na maendeleo,huku tukijua kwamba uchaguzi ni shughuli muhimu inayofanywa katika
kupiga kura na kupigiwa kura hivyo suala la amani wakati wote wa uchaguzi ni
muhimu kwa ustawi wa taifa ‘’
Awali
mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Arusha( APC)Cloud Gwandu
ameishukuru Taasisi ya Mwalimu Nyerere(MNF) kwa kutoa warsha hiyo ya mafunzo
kwa waandishi wa habari itakayowasaidia kuwajengea uwezo wa kuripoti kipindi chote
cha uchaguzi mkuu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...