Wataalamu wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Save a Child’s Heart (SACH) wa nchini Israel na Ujerumani wakiwa katika sehemu mbalimbali za hifadhi ya Ngorongoro wakati wa utalii wa kitabibu uliofanywa na wataalamu hao. Utalii wa kitabibu kwa madaktari hao ni fursa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli.

Picha na: Genofeva Matemu – JKCI

*******************************

Na: Genofeva Matemu – JKCI

Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Save a Child’s Heart (SACH) lenye wataalamu wa afya kutoka nchini Israel na Ujerumani wapata fursa kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kufanya utalii wa kitabibu katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.

Utalii huo wa kitabibu umeanza kufanyika mara baada ya kambi maalumu ya matibabu ya moyo ya siku tano iliyofanywa na madaktari hao kwa kuwafanyia watoto 18 upasuaji mdogo wa kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba katika taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hifadhi Ngorongoro Mkuu wa kitengo cha Tafiti na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka JKCI Naiz Majani amesema kuwa JKCI imekuwa ikishirikiana na shirika la SACH tangu mwaka 2008 kwa kuwatiba watoto, kutoa vifaa vya matibabu kwa watoto pamoja na kuwasafirisha baadhi ya watoto kwenda nchini Israel kwa ajili ya matibabu makubwa ya moyo.

Dkt. Naiz amesema kuwa mwaka 2019 SACH wakiwa katika muendelezo wa kambi maalum ya matibabu kwa watoto pale JKCI walipata bahati ya kukutana na Mhe. Rais ambaye alifurahia kazi ambazo wanazifanya pamoja na mchango wao wa vifaa tiba kwa ajili ya kuhimarisha huduma za afya hasa upande wa magonjwa ya moyo hivyo kuwaahidi kutembelea na kuona vuvutio tulivyonavyo hapa nchini.

“Uwepo wa madaktari kutoka shirika la SACH hapa nchini umesaidia sana kwani huko nyuma tulikua hatuna uwezo mkubwa sana wa kufanya matibabu ya moyo hapa nchini hivyo kuwapeleka watoto nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ambayo yalikua ni ya gharama kubwa kwani mtoto mmoja alitibiwa kwa gharama ya kati ya milioni 30 hadi 40 kwa baadhi ya magonjwa ya moyo, lkn kwa kuweza kufanya matibabu ya moyo hapa nchini gharama za matibabu kwa mtoto mmoja zimeweza kushuka hadi kufikia milioni sita hadi nane kwa baadhi ya magonjwa ya moyo” alisema Dkt. Naiz.

“Kuja kwa madaktari wa SACH hapa nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya matibabu ya moyo kwa watoto ni kwa kujitolea hivyo wamefurahishwa sana na nafasi hii ambayo Mhe, Rais John Pombe Magufuli ameitoa kwao kutembelea hifadhi ya taifa ya Ngorongoro” alisema Dkt. Naiz.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro Fredy Manongi amesema kuwa ujio wa wataalamu wa afya kutoka JKCI pamoja na wenzao kutoka nchini Israel na Ujerumani ni njia mojawapo ya kupanua masoko ya kitalii hapa nchini kuweza kupata wageni wengi zaidi kutoka nchi za Israel na ujerumani.

“Ngorongoro ni eneo la urithi wa dunia, ni eneo la milima na mabonde linalotambulika na UNESCO, lakini pia ni eneo lenye uwepo wa bonde la ngorongoro ambalo limekua eneo muhimu sana kwa wanyamapori hivyo matumaini yetu makubwa baada ya wageni hawa kutembelea hifadhi hii ni pamoja na ongezeko la watalii kutoka nchi ya Israel na Ujerumani” alisema Bw. Manongi.

Naye Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka shirika la SACH Assa Sagi amesema kuwa ukarimu alioufanya Mhe. Rais Magufuli kwa wataalamu hao ni wa kipekee hivyo kuahidi kuendelea kutembelea vivutio vingine vilivyopo hapa nchini wakati wanapokuja kwa ajili ya kambi maalum za matibabu ya
moyo.

Toka JKCI imeanza kufanya kambi maalum za matibabu ya moyo na shirika SACH mwaka 2008 wameweza kuhudumia karibu watoto 300 wenye magonjwa ya moyo,
kuwapeleka watoto karibu 75 wenye matatizo makubwa zaidi ya moyo kutibiwa nchini Israel na kwa kipindi hiki cha wiki moja kwa mwaka 2020 wameweza kuhudumia watoto 18 na wengine 10 wapo katika hatua ya kupelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu makubwa ya moyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...