Na Karama Kenyunko, globu ya jamii

MSHTAKIWA mmoja katika kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa kupambana na mauaji ya Tembo, Wayne Lotter amezimia mahakamani huku mwenzake akiieleza mahakama kuwa, raia wa kigeni katika kesi hiyo  wanaoishi gereza la keko wamenyimwa chakula kwa siku tano na kupelekea hali yao kudhoofu.

Mshtakiwa Ndimana Zebadayo ambaye ni raia wa Burundi amedai hayo leo Januari 17,2020 wakati kesi hiyo inayomkabili yeye pamoja na wenzake 17 ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.
Mapema wakili wa Serikali Easter Martin amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi, Godfrey Isaya kuwa Kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa kwani upelelezi bado haujakamilika na jalada la kesi liko kwa DPP.

 Awali kabla washtakiwa hao walipotakiwa kupanda kizimbani, mshtakiwa Habonimana Nyandwi raia wa Burundi, alishindwa kusimama na kudondoka chini huku akionekana kugeuza macho, ndipo askari polisi waliokuwa karibu walimsogelea na kumvua viatu pamoja na mkanda.

Kufuatia hali hiyo, washtakiwa wenzake walipanda kizimbani ndipo mshtakiwa Zebadayo aliponyoosha mkono huku akiangua kilio kwa nguvu na kudai, raia wa kigeni waliopo  kwenye kesi hiyo hawajui ushiriki wao lakini hawana ndugu wala mtu yeyeto wa kuwaona wala kuwapa chakula.

"Tumedhoofika hatuna ndugu wa kutuletea chakula hapa nchini na gerezani tunanyimwa chakula leo siku ya tano, tumekatiwa huduma ya chakula kam raia wa kigeni.

Akijibu hoja hizo, wakili Easter amedai, mahabusu wanapatiwa huduma zote za chakula pamoja na malazi. Magereza, hivyo kuhusu hilo suala ni vema, wakaulizwa Magareza. Ila upelelezi uko hatua za mwisho, jalada lipo kwa Dpp kwa ajili ya kulisoma.

Hata hivyo, askari magereza alipoulizwa juu watuhumiwa hao kutopewa chakula alidai kuwa hana taarifa zozote kwa anachojua yeye mahabusu wote wanapata chakula.

Naye, mshtakiwa Ayubu selemani amedai, katika mahabusu ya keko kuna raia wa kigeni wengi na wote wanapata chakula kwa wakati isipokuwa wawili hao waliopo kwenye kesi hiyo ambapo wamekatiwa huduma
Siku tano ambapo amedai waliitwa na afisa usalama wa keko na kuambiwa kuwa hawatapewa hicho chakula Malibu kwa rais wa kigeni. Ameongeza kuwa wakijitahidi kwenda kumuona bwana jela kupeleka malalamiko yaoa lakini askari hao wa kawaida wakawa wanawazuia.

Amedai kuwa, ni jana ndio  walifanikiwa kumuona bwana jela ambaye naye aliwaambiwa washtakiwa hao ni majirani zetu hawawezi kupewa hicho chakula.
Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Isaya ameahirisha kesi hiyo kwa siku saba yaani itatajwa tena Januari 24,2020 ili kupata taarifa zaidi juu ya malalamiko ya washtakiwa hao.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya mauaji namba 9 ya mwaka 2017 ni raia wa Burundi Habonimana Nyandwi na Nduimana Jonas maarufu Mchungaji (40) mkazi wa Kamenge Burundi,Robert Mwaipyana

Wengine ni Godfrey Salamba (42) mkazi wa Kinondoni Msisiri A. Inocent Kimaro (23) mkazi wa Temeke Mikoroshini, Chambie Ally (32) mkazi wa Kia/Boma na Ofisa wa NBC, Robert Mwaipyana (31) mkazi wa Temeke Mikoroshini.

Wengine ni Meneja wa Benki ya Backlays, Khalid Mwinyi (33) mkazi wa Mikocheni B, Rahma Almas (37) mkazi wa Mbagala B na Mohammed Maganga (61) mchimba makaburi, Allan Mafue, Ismail Mohammed, Leornad Makoye, Amino Sham, Ayoub Selemani, Joseph Lukoa, Gaudence Matemu na Abuu Mkingie.

Katika kesi ya msingi washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Julai Mosi na Agosti 16, 2017 walikula njama ya kufanya mauaji ya Lotter.

Katika shtaka la pili, washtakiwa hao wanadaiwa Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie iliyopo wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, wanadaiwa kumuua Lotter.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...