Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga
mkoani Rukwa Khalfan Haule (kulia) akimueleza jambo Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati
alipokwenda kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za Makazi katika Manispaa
ya Sumbawanga mkoa wa Rukwa jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Muungano Saguya.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya
Sumbawanga mkoani Rukwa Khalfan Haule (kulia) wakati alipokwenda kukagua
mradi wa ujenzi wa nyumba za Makazi katika Manispaa ya Sumbawanga mkoa
wa Rukwa jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni Meneja Mawasiliano wa Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC) Muungano Saguya.(PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
……………..
Na Munir Shemweta, WANMM RUKWA
Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) kuhakikisha inakamilisha mradi wake wa ujenzi wa nyumba za Makazi
za Jangwani katika Manispaa ya Sumbawanga mkoa wa Rukwa katika kipindi
cha mwaka huu wa fedha 2019/2020.
Akizungumza
wakati akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba hizo za makazi
wenye jumla ya nyumba ishirini za ghorofa moja jana katika Manispaa ya
Sumbawanga mkoa wa Rukwa Naibu Waziri Mabula alisema mradi huo lazima
ukamilishwe mapema kwa kuwa fedha iliyotumika ni nyingi.
Kauli hiyo ya
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inafuatia kuelezwa
na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo kuwa mradi huo umekuwa
ukimsumbua kutokana na kuchukua muda mrefu bila kukamilika na hivyo
kuufanya mkoa kutojua hatma yake wakati uhitaji wa nyumba za kupanga
katika manispaa ya Sumbawanga ni mkubwa.
‘’ Naungana na RC
kuwa mradi huu umechukua muda mrefu hivyo ni lazima uishe katika mwaka
huu wa fedha wa kiserikali na April mwaka huu 2020 narudi hapa
Sumbawanga’’ alisema Dkt Mabula.
Kwa mujibu wa
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Muungano Saguya,
mradi huo wa ujenzi wa nyumba za Makazi Jangwani katika Manispaa ya
Sumbawanga ulianza mwezi Juni 2014 na ulisimama kupisha uchunguzi baada
ya kuwepo tuhuma za ubadhilifu kwenye mradi huo.
Hata hivyo,
Saguya alisema kiasi cha shilingi milioni 366.2 kinahitahika kumalizia
mradi huo na tayari Shirika lake limejipanga na maandalizi kwa ajili ya
ukamilishaji mradi yamekamilika na muda wowote umaliziaji nyumba hizo
utaanza.
Mradi huo wa
Nyumba za Makazi Jangwani katika Manispaa ya Sumbawanga mkoa wa Rukwa
ambao nyumba moja ilishanunuliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHF)
zikikikamilika zitapangishwa na zitaweza kuliingizia Shirika la Nyumba
la Taifa kiasi cha shilingi 5,400,000 kila mwezi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...