Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Nakala ya Mpango
Kabambe wa Mji wa Tunduma 2015-2035 Kaimu Mkurugezi wa Halmashauri ya
Mji wa Tumduma Lusajo Mwalukasa jana wakati wa uzinduzi wa Mpango huo
katika Mji wa Tunduma wilaya ya Momba mkoa wa Songwe.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Nakala ya Mpango
Kabambe wa Mji wa Tunduma 2015-2035 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa
Tunduma Ally Mwafongo jana wakati wa uzinduzi wa Mpango huo katika Mji
wa Tunduma wilaya ya Momba mkoa wa Songwe.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Nakala ya Mpango
Kabambe wa Mji wa Tunduma 2015-2035 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia
Jenerali Mstaafu Nicodemus Mwangela jana wakati wa uzinduzi wa Mpango
huo katika Mji wa Tunduma wilaya ya Momba mkoa wa Songwe (PICHA NA
WIZARA YA ARDHI)
……………..
Na Munir Shemweta, WANMM TUNDUMA
Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezindua Mpango
Kabambe wa miaka ishirini (2015-2035) wa Mji wa Tunduma katika mkoa wa
Songwe na kuzitaka halmashaur zote nchini ambazo hazijaadaa mipango
kabambe katika Miji yao kuandaa mpango kabambe ili kuongeza kasi ya
kupanga na kupima miji yote Tanzania .
Naibu Waziri
Mabula amezindua Mpango huo Kabambe wa Mji wa Tunduma jana katika mji wa
Tunduma wilaya ya Momba mkoa wa Songwe wakati akiwa katika ziara yake
ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi pamoja na kukagua utekelezaji
wa miradi ya ujenzi inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Alisema,
kukamilika kwa mpango kabambe wa mji wa Tunduma kumekuja wakati muafaka
kwa kuwa mpango huo utachochea utumiaji fursa na rasilimali zilizopo
Tunduma na kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi
sambamba na kupunguza au kumaliza migogoro ya ardhi.
‘’Mpango huu
utachochea utekelezaji wa malengo ya muda mrefu ya serikali ya kuwa na
uchumi wa kati wa viwanda na hii inajidhihirisha katika mpango kabambe
wa Mji wa Tunduma pale jumla ya hekta 4190 sawa na asilimia kumi ya
maeneo yaliyopangwa kwa matumizi ya ardhi zimetengwa kwa ajili ya
viwanda’’ alisema Waziri Mabula.
Alitoa wito kwa
Halmashauri na wadau wa maendeleo katika mji wa Tunduma kuandaa mkakati
wa mpango kazi wa utekelezaji Mpango Kabambe sambamba na kutafuta wabia
na wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali
zilizoainishwa katika Mpango huo.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemus Mwangela
alisema Mapango Kabambe wa Mji wa Tunduma ni muhimu kwa mji huo kwa kuwa
uko mpakani na una shughuli nyingi huku asilimia sabini ya mizigo
ikipitia katika mji huo.
Alisema, Mji wa
Tunduma unahitaji kutazamwa kwa macho mawili kwa kuwa muingiliano wa
wananchi wa Tanzania na nchi za SADC ni mwingi na kusisitiza katika mkoa
wake Mji wa Tunduma ni wa kwanza kuandaa Mpango Kabambe.
Akielezea Mpango
huo Kabambe wa Mji wa Tunduma, Katibu Tawala wa wilaya ya Momba Mery
Marcko alisema, lengo la mpango huo ni kuwa kitovu cha biashara kwenye
mkoa wa Songwe, Nyanda za Juu Kusini na Nchi za Kusini mwa Jangwa la
Sahara na kutaja maeneo ya kimkakati kuwa ni Kati Kati ya Mji wa
Tunduma, Miji ndani ya Mji yaani Satellite Towns, Ukanda Maalum wa
Kibiashara na Ukanda wa Viwanda.
Kwa mujibu wa
Katibu Tawala wa Wilaya ya Momba, jumla ya miradi 24 itatekelezwa katika
awamu ya kwanza (2015-2020) na kuitaja baadhi yake kuwa ni Kituo cha
Mabasi cha Mpemba ambacho ujenzi wake umeanza, Barabara ya lami kutoka
Mpemba hadi Isongole itakayounganisha eneo la Mpemba na nchi jirani ya
Malawi kupitia Isongole (Ileje), Ujenzi wa hospitali ya Mji wa Tunduma
na ukamilishaji ujenzi wa miundo mbinu ya maji pamoja na ujenzi wa
maegesho ya malori unaojengwa katika kata ya Chapwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...