Na. Catherine Sungura-Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kuipatia kiasi cha shilingi bilioni mbili hospitali ya rufaa ya kanda KCMC ili kuweza kutoa huduma za tiba za mionzi hospitalini hapo.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akijibu maswali kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii jijini hapo.

“Tumekubaliana na Katibu Mkuu kuitafuta hiyo bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mionzi (bunker) kwa hospitali hii tutawapatia".

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa wizara yake inayo muelekeo kwa hospitali zote za rufaa za kanda kutoa huduma za mionzi hivyo hakutakuwa na haja ya wagonjwa wa kanda ya kaskazini kusafiri hadi Ocean road kupata huduma za mionzi.

"Wizara tumeanza kutoa huduma za mionzi,mwaka jana tulizindua hospitali ya Bugando,lengo letu ni kuweka huduma hizi kwenye hospitali zote za rufaa za kanda kama Mbeya  na tunafikiria kuweka na hapa kwenye hosputali ya Benjamin Mkapa".Alisisitiza Waziri Ummy

Hata hivyo Waziri Ummy  amesema wizara imeweza kuwapatia hospitali ya KCMC fedha kwa ajili ya watumishi pamoja na dawa kiasi cha shilingi bilioni 5 katika kipindi cha miezi sita."Kama serikali itaendelea kuthamini suala la ubia katika utoaji wa huduma za afya na mashirika ya dini na watu binafsi".

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC Dkt. Gilliard Masenga amesema kuwa asilimia sitini ya wagonjwa wa saratani wanahitaji huduma ya mionzi na hospitali  hiyo imeweza kuona jumla ya wagonjwa 4323 kwa kipindi cha mwaka jana na kufanya uchunguzi wa magonjwa ya saratani ambapo kati yao watoto 239 na watu wazima ni 4084,aidha wamefanya kampeni maalum ya upimaji na ushauri katika wilaya ya Arumeru na watu 307 walipatiwa huduma ya uchunguzi wa awali wa saratani. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akijibu maswali kwenye kamati hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya rufaa ya kanda KCMC Dkt. Gilliard Masenga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya hospitali ya KCMC kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii.
  Wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii wakati wa kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya hospitali ya KCMC na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii wakifuatilia taarifa kutoka hospitali hizo mbili .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...