Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.
MEYA wa Ubungo, Boniface Jacob ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wimbo wa Harambe Harambe unaotumiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), wakati wa kampeni unalenga kuwahamasisha wananchi ila unawanyima kura upande wa wapinzani.

Hayo yameelezwa leo Januari 22,2020 na Jacob ambaye  ni shahidi wa kumi wa upande wa utetezi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akitoa ushahidi katika kesi ya uchochezi inayowakabili vigogo tisa wa Chadema ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Akiongozwa na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala, kutoa ushahidi wake Jacob alidai wimbo uliuoimbwa na marehemu Kapteni John Komba kupitia bendi ya TOT na chama hicho kinapofanya mikutano yake ya chama ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Rais John Magufuli na  kampeni hauimbwi vizuri.

Aliutaja wimbo huo "Harambe mara tatu, wapinzani tuwalete, tuwachane chane tuwatupe, CCM tuwalete tuwakumbatie tuwabusu,".

Hata hivyo, shahidi huyo aliulizwa maana ya wimbo huo swali ambalo lilipingwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alipinga swali ambalo baada ya mabishano mafupi Hakimu aliruhusu kuulizwa ndipo shahidi huyo alidai  wimbo huo unamaanisha kuwanyima kura wapinzani.

Akiendelea kutoa ushahidi wake, Jacob alidai Februari 16, 2018 majira ya asubuhi Mkurugenzi wa Kinondoni, Aron Kagurumjuli alikula kiapo kuwa Wakala Mkuu wa Uchaguzi kwa Chadema na kwamba ndiye alikuwa mshehereshaji kwenye mkutano wa kufunga kampeni wa chama hicho uliofanyika Viwanja vya Buibui Mwananyamala, Dar es Salaam.

Alidai wazungumzaji wakuu katika mkutano huo alikuwa Mbowe aliyezungumza kwa dakika 30 kuhamasisha watu kujitokeza kupiga kura pamoja na mgombea wa Ubunge kwenye uchaguzi mdogo,Salum Mwalimu ambaye alizungumza kwa dakika 20 akiomba kura na kueleza kwanini anania ya kuongoza jimbo hilo.

Alidai wabunge wengine waliopata nafasi ya kusalimia umma uliokusanyika kwenye mkutano huo ni Halima Mdee (Kawe), Peter Msigwa (Iringa Mjini) ambaye alidai alihamasisha wananchi kufanya mabadiliko, John Heche (Tarime Vijijini) ambaye alihamasisha vijana kuwa na mwamko wa kupiga kura siku ya uchaguzi.

Alidai baada ya mkutano huo kwisha, viongozi hao waliondoka na magari yao wakisindikizwa na maofisa wa polisi ambao walikuwa wanalinda mkutano huo ili ufanyike kwa amani.

Hata hivyo alidai kuwa,hawajawahi kupokea malalamiko yoyote kutoka kwa Mwananchi kuhusiana na hotuba ilitolewana Viongozi wa Chadema katika mkutano huo bali   walipongezwa na wananchi.

Pia alidai, kupitia hotuba hizo za viongozi wa Chadema wananchi walihamasika kwenda Kupiga kura.

Katika swali jingine, Wakili Peter Kibatala alimuuliza Jacob katika lugha wakati wa uchaguzi kuna kuchinja na kichinjio unaizungumziaje hiyo,Jacob alidai kuwa Kuchinja ni kumnyima mgombea kura na kichinjio ni kadi ya kupigia kura.

Washitakiwa wengine  katika kesi hiyo ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Iringa Mjini,  Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Dk Vincent Mashinji.

Washitakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...