Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) George Simbachawene akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa za
Utekelezaji wa majukumu na bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kipindi cha Julai- Desemba 2019 kilichofanyika bungeni jijini Dodoma leo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa za Utekelezaji wa majukumu na bajetiya Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kipindi cha Julai-Desemba 2019 kilichofanyika bungeni jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akifafanua jambo katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa majukumu na bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kipindi cha Julai-Desemba 2019 kilichofanyika bungenijijini Dodoma leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumuya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kilichofanyika bungeni jijini Dodoma leo.
Sehemu ya watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakifuatilia kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira bungeni kilichofanyikajijini Dodoma leo.

******************************

Lulu Mussa na Robert Hokororo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) George Simbachawene amesema Serikali imefanya mapitio ya Sera ya Mazingira ya mwaka1997 ili kuzingatia changamoto mpya za kimazingira zinazojitokeza mara kwa mara.

Akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu na Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimazi wa Mazingira (NEMC) kwa kipindi chaJulai – Desemba 2019 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira amesema Ofisi imeendelea kuratibu utekelezaji wa Sera ya Taifa yaMazingira ya Mwaka 1997 pamoja na Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.

Simbachawene amesema Rasimu ya Mwongozo wa mita 60 katika kuhifadhi vyanzo vya maji katika bahari, maziwa na mito imeandaliwa; Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2020 imeandaliwa na ipo katika hatua ya
kuwasilishwa katika vyombo vya maamuzi; na Itifaki ya SADC ya Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo Endelevu iliridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Rasimu ya Mwongozo wa Uwekezaji katika usimamizi wa Taka imeandaliwa; Kanuni za Usumamizi wa Taka za kielekroniki za mwaka 2019 zimeandaliwa; Kanuni za Usimamizi wa Taka hatarishi za mwaka 2009 zimepitiwa na Mwongozo wa Kitaifa wa kufanya tathmini ufuatiliaji na utoaji taarifa za hewa ukaa umeandaliwa” Simbachene alisisitiza.

Awali, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo amesema Ofisi hiyo inatarajia kuandaa mkutano mkubwa utakaowakutanisha viongozi kutoka Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzungumzia agenda ya Mazingira ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za utunzaji wa mazingira nchini.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka amesema Baraza linaendelea na Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira kwa kufanya Kaguzi za Mazingira.

“Baraza limefanya ukaguzi katika miradi 870 ili kuhakikisha uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira nchini. Vilevile. Kaguzi hizo zilifanyika katika shughuli za kiuchumi na kijamii zenye kuweza kuleta athari kwa mazingira” Gwamaka alisisitiza.

Kuhusu Udhibiti wa Taka Hatarishi, Baraza kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za Serikali lilishiriki katika zoezi la ukaguzi wa makontena 151 ya chuma chakavu yaliyokuwa yanatakiwa kusafirishwa nje ya nchi ikiwa ni kujua uhalali wa kuendesha biashara hiyo na kukagua shehena ya makontena hayo ili kubaini aina ya chuma chakavu kilichopo ndani ya makontena.

Aidha, hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 ikiwemo kutozwa faini, zilichuliwa dhidi ya Makampuni yaliyokaguliwa na kukutwa na makosa.

Dkt. Gwamaka amesema kuwa Baraza limesajili jumla ya Miradi 664 (Miradi 387 ya Tathmini za Athari kwa Mazingira na Miradi 277 ya kufanyiwa Ukaguzi wa Athari za Mazingira) ikiwa ni asilimia 55 ya miradi ambayo imekusudiwa kufanyiwa mapitio.

kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20. Kwa kipindi hicho miradi ipatayo 375 imeidhinishwa kupata vyeti, hii ikiwa miradi 225 kwa ajili ya Tathmini za Athari kwaMazingira (Environmental Impact Assessment) na Miradi 150 Kwa ajili ya Ukaguzi wa Athari za Mazingira (Environmental Audit). Aidha miradi mingine ipo katika hatua tofauti za upembuzi.

Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jitu Vrajlal Son ameshauri Serikali kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ya mazingira katika ngazi zote za Serikali na kuhimiza uanzishaji waMfuko wa mazingira nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...