Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
BAADA ya familia kukutana  na kujadili suala la mwanamfalme wa Uingereza Prince Harry na mkewe Meghan kujiondoa katika shughuli za kifalme, Malkia Elizabeth  ametoa maelezo ikiwemo kuendelea kushirikiana na wawili hao katika maisha mapya  wanayoenda kuyaanza ambapo watakuwa wakiishi nchini Canada na Uingereza.

Maelezo yaliyotolewa na Malkia Elizabeth ni pamoja na kama familia kuridhia uamuzi wa mjukuu (Prince Harry) na mkewe Meghan kujiengua katika nyadhifa za kifalme na kuishi kwa kujietegemea wenyewe na kueleza kuwa familia ilitamani wanandoa hao kubaki na kutekeleza majukumu yao ya kifalme  lakini wameheshimu uamuzi wao wa kutaka kuanza maisha mapya ya kujitegemea wao wenyewe.

Awali wanandoa hao (Harry na Meghan) walieleza kuwa hawatotegemea Fedha za umma katika maisha yao mapya badala yake watajitegemea kiuchumi.

Pia Malkia amesema kuwa hayo mi masuala ya kifamilia na ni ngumu sana kufikia tamati na kusema kuwa uamuzi kuhusiana na jambo hilo ufanyike kwa siku zijazo.

Kwa upande wa Canada nchi ambayo wawili hao wamependelea kuishi Waziri Mkuu nchini humo Justin Trudeau amesema mazungumzo yanahitajika kuhusiana na gharama za usalama kwa wawili hao na hiyo ni pamoja na ulinzi na mipango mingine.

Taifa la Uingereza linaundwa na mataifa ya North Island, England, Scotland na Wales huku likiwa taifa la utawala wa ufalme wa kikatiba (Monarch) linalofuata mfumo wa utawala wa bunge.

Mwanamfalme Harry akiwa ni moja ya wanaotegemewa kurithi nafasi ya Malkia Elizabeth na kujiondoa kwake kumezusha maswali mengi na hiyo ni kutokana na kufahamika kwake hasa katika ushiriki wake katika jeshi la Uingereza akiwa Mwanamfalme wa kwanza kutoka familia ya tajiri kwenda vitani mara mbili.

Wanahistoria na wachambuzi wanadai kuwa mwanamfalme Harry baada ya kutoona uelekeo wa kuchukua nafasi ya ufalme na imepelekea  kufikia maamuzi ya kuachana na familia ya kifalme na kubaki kama watu wa kawaida ila kwa kuendelea kutoa mchango wao kwa familia hiyo.

Licha ya familia ya kifalme kueleza kusikitishwa na maamuzi kwa kusema imekua ndoto huku wakihoji itakuwaje kuhusu suala la ulinzi wao itakuaje.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...