Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali Bw.Chotto Sendo akizungumza wakati wa kikao cha wadau kuhusu rasimu ya taarifa ya tathmini ya utayari wa sekta ya umma Tanzania kutumia Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali (ISO 55000 Series) Jijini Dodoma.
Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Balandya Elikana ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Adolph Ndunguru, akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kuhusu rasimu ya taarifa ya tathmini ya utayari wa sekta ya umma Tanzania kutumia Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali (ISO 55000 Series) Jijini Dodoma.
Washiriki wa kikao cha wadau kuhusu rasimu ya taarifa ya tathmini ya utayari wa Sekta ya Umma Tanzania kutumia Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali (ISO 55000 Series) wakichukua taarifa muhimu wakati kikao hicho kikiendelea katika ukumbi wa Kilimanjaro wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Balandya Elikana akiteta jambo na Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma wizarani hapo Dkt. Fredrick Mwakibinga wakati wa kikao cha wadau kuhusu rasimu ya taarifa ya tathmini ya utayari wa Sekta ya Umma Tanzania kutumia Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali (ISO 55000 Series) kilichofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro wizarani hapo Jijini Dodoma.
Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Fredrick Mwakibinga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha wadau kuhusu rasimu ya taarifa ya tathmini ya utayari wa sekta ya umma Tanzania kutumia Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali (ISO 55000 Series), kilichofanyika jijini, Dodoma.
Meza Kuu ikiongozwa na Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Balandya Elikana (katikati) wakiwa katika kikao cha wadau kuhusu rasimu ya taarifa ya tathmini ya utayari wa Sekta ya Umma Tanzania kutumia Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali (ISO 55000 Series) kilichofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro wizarani hapo Jijini Dodoma

Waandaaji wa kikao cha wadau kuhusu rasimu ya taarifa ya tathmini ya utayari wa Sekta ya Umma Tanzania kutumia Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali (ISO 55000 Series) wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea katika ukumbi wa Kilimanjaro wizarani hapo Jijini Dodoma



Washiriki wa kikao cha wadau kuhusu rasimu ya taarifa ya tathmini ya utayari wa Sekta ya Umma Tanzania kutumia Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali (ISO 55000 Series) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa kikao hicho Jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

………………….

Na Farida Ramadhani, Dodoma

Tanzania ipo katika hatua za mwisho za kuanza rasmi kurasimisha Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali (ISO 55000 Series) ili kuongeza ufanisi na ubora katika usimamizi wa mali za Umma.

Hayo yameelezwa na Kaimu Kamishna wa Bajeti, Bw. Balandya Elikana kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, katika uzinduzi wa kikao cha kukusanya maoni ya wadau kuhusu taarifa ya tathmini ya utayari wa Sekta ya Umma Tanzania kutumia mfumo wa Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali (ISO 55000 Series).

Bw. Elikana alisema kuwa Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali vinalenga kutoa muongozo katika sekta ya Usimamizi wa Mali za Umma kwa kuainisha mahitaji muhimu ya usimamizi wa mali za Umma pamoja na namna bora ya usimamizi wa mali hizo.

“Utumiaji wa Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali ni muhimu kwa Tanzania hususan katika kipindi hiki ambacho nchi ipo katika harakati za kuwa na uchumi wa kati”alisema Bw. Elikana

Alibainisha kuwa kwa kulitambua hilo, Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na wadau pamoja na Washirika wa Maendeleo kupitia Mradi wa Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP) imefanya tathmini na kuandaa mpango wa utumiaji wa viwango vya kimataifa katika usimamizi wa mali.

“Leo ni sehemu ya kukamilisha kazi kwa kukusanya maoni ya wadau na kuyachambua ili kuweza kuboresha rasimu ya taarifa ya tathmini iliyofanyika pamoja na mpango kazi ambao Tanzania itaufuata katika kutumia Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali”, alifafanua Bw. Elikana.

Alisema kuwa Tanzania itapata faida mbalimbali kwa kufuata viwango vya kimataifa vya usimamizi wa mali ikiwemo, kuimarisha usimamizi wa Mali na kufanya ulinganifu wa Usimamizi wa Mali kwa Viwango vya Kimataifa pamoja na kurahisisha uwekaji wa vipaumbele kwenye usimamizi wa mali husika.

Bw. Elikana alisema faida nyingine ni kupunguza gharama ya matengenezo ya mali, kuboresha utoaji huduma, kurahisisha utoaji wa maamuzi, kurahisisha ukaguzi wa vihatarishi pamoja na kuendana na mahitaji ya viwango vingine vya kimataifa.

“Usimamizi wa mali za umma ni wajibu wa kila mwananchi na linapaswa kutekelezwa kwa uadilifu na kwa weledi mkubwa, na ninatoa wito kwa washiriki wote katika kikao hiki kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha tathmini na mpango kazi ulioandaliwa”alisisitiza Bw. Elikana.

Naye Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Chotto Sendo alisema kuwa usimamizi wa mali za Serikali ni jukumu la muhimu kwa maendeleo ya nchi na Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali vitaongeza ufanisi.

“Usimamizi wa mali za Serikali umeanza muda mrefu lakini suala la utumiaji wa mifumo ya usimamizi huo bado haijaanza kutumika kikamilifu, kuanza kutumika kwa Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali kutaleta ahueni”, alifafanua.

Kwa upande wake Kamishana wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Frederick Mwakibinga, alisema kuwa uwekezaji wa Serikali ni mkubwa na anaamini maoni ya kikao hicho yatasaidia kutatua baadhi ya changamoto za usimamizi wa mali hizo.

Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali vilitangazwa rasmi kuwa sehemu ya viwango vya kimataifa na Shirikisho la Viwango vya Kimataifa (International Organisation for Standardisation) mwaka 2014 baada ya kuridhishwa na nchi wanachama 32, na kwa sasa viwango hivyo vinatumika kwenye nchi zaidi ya 41 ikiwemo Botswana, Japan, India, Canada na Uingereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...