Na Yassir Simba, Globu ya jamii 

MOJA ya Wanzania ambao walipata nafasi ya majina yao kusikika na kutamba kwa kiwango kikubwa katika medani ya mchezo wa kikapu nchini Tanzania basi ni pamoja na kijana Hasheem Thabeet. Ndio, Hasheem alitikisa katika mchezo huo. Watanzania wakamjua, Afrika Mashariki ikamuelewa na Dunia ya mchezo huo ikamfahamu yeye na uwezo wake. Alikuwa na kipaji cha hali ya juu kilichoendana na bahati. 

Kwa Hasheem Thabeet kwake haikuwa kazi ngumu kwenda nchini Marekani kwenye ligi bora kabisa ya mchezo huo. Yaani kwa uwezo aliokuwa nao alitoka Sekondari ya Makongo jijini Dar es Salaam na kisha kutua katika Ligi ya NBA. Kabla ya kuendelea zaidi, naomba nieleze kidogo kuhusu NBA na kisha tutaendelea na kile ambacho kimenisukuma kumuelezea Hasheem Thabeet. 

Iko hivi Juni mwaka 1946 katika Jiji la New York nchini Marekani ilianziswa ligi ya mpira wa kikapu maarufu duniani ikatambulika kama NBA (National Basketball Association), ikishirikisha timu kama Los Angeles Lakers na Golden State Warriors. Timu nyingine ni Indiana Fever, Chicago Sky,Phoenix, Minnesota Lynx,Los Angeles Sparks,Chicago Bulls,Miami heat na nyengine kibao. Unapozungumzia NBA kwenye mchezo huo maana yake unazungumzia ligi yenye umaarufu mkubwa duniani na ndio yenye mastaa kibao. 

Hivyo Hasheem naye alikuwa moja ya mastaa kwenye ligi hiyo. Hakuwa wa kawaida. Taarifa za Hasheem kuwamo kwenye NBA zilimsisimua kila Mtanzania. Tulijiona wenye bahati ya hali ya juu. Sasa tuendelee, mwaka 2009, Hasheem Thabeet aliyekuwa nyota wa mpira wa kikapu kutoka Tanzania alisimama katika majukwaa ya uwanja Allen County War Memorial Coliseum ya klabu ya Fort Wayne Mad Ants na kusalimiana na umati mkubwa wa takribani mashabiki 130000 uliojitokeza usiku huo. Usiku huo ulikuwa na maana kubwa katika mchezo wa kikapu hasa kwa wachezaji a Tanzania wakiwamo waliokuwa wanacheza na Hasheem.

Ndio usiku ambao ulifufua matumaini ya wachezaji wa mpira huo kwamba inawezekana. Kama Hasheem amekwenda nao iko siku watakwenda NBA. Watanzania wakawa wanafuatilia NBA na hasa siku ambazo timu ya Hasheem ilikuwa inacheza. Ndiko ambako na sisi wengine tukawafahamu hao mastaa wa Ligi hiyo achilia mbali wa Michael Jordan, William Athony Parker na Cobe Brayant. Hata hivyo katika ligi ya NBA Hasheem Thabeet alidumu kwa miaka mtano tu. Wakati anajiunga na ligi hiyo alitabiriwa makubwa lakini ikawa kinyume chake. Ukweli uko hivi uwezo wa Hasheem Thabeet ulianza kupungua kabla ya muda huo. Ziko sababu nyingi za kufanya vibaya.

Kwa leo naomba nitaje mbili na zikibaki siku nyingine tukipata nafasi. Sababu ya kwanza inatajwa kuwa ni utovu wa nidhamu na sababu ya pili ni ile ya kutumia muda mwingi kwa maisha yake binafsi kuliko mchezo, sababu zilizoainishwa na Kocha wake Damon Stoudamire kupitia mtandao wa BR MAG. Wakati uwezo wake unaanza kupungua aliondolewa kwenye timu ya Wayne kwenda Indiana na huko nako hali haikuwa shwari kwake. Mengi yakaanza kuzungumza dhidi yake na mashabiki na wapenzi wa mchezo huo.

Tunafamu Hasheem alianza kuwika kwenye mchezo huo akiwa na umri wa miaka 15. Ilifika hatua Hasheem akawa analalamikiwa kwa kutopokea simu za muhimu alizokuwa anapigiwa na viongozi wa timu yake. Hakuwa anajali kabisa na matokeo yake akakumbwa a kashfa ya utovu wa nidhamu. 

Kwa sasa Hasheem Thabeet bado yupo nchini Marekani lakini sio tena kwenye ule ulimwengu wa mchezo huo. Hasikiki tena na hakuna anayefuatilia kutaka kujua anafanya nini. Najua huu si wakati wa kuendelea kumtupia lawama Hasheem huenda kuna mambo yaliyomsibu hadi kufika hapo alipofika. 

Iko siku atasimulia mwenyewe. 

Hata hivyo kuna mambo ya kujifunza. Ukiwa na kipaji hasa kwenye ulimwengu wa michezo, tambua kwamba kweli unacho kipaji na jinsi gani utahakikisha unakilinda. Ni maoni yangu Hasheem alitambua anacho kipaji lakini alishindwa kukilinda. Ametamba katika kipindi kifupi sana. 

Nidhamu nayo ni muhimu katika eneo lolote lile. Iwe kwenye michezo ama kazi nyingine yoyote.Hasheem aliondoka mwenye nidhamu akiwa Makongo na baada ya kufika NBA nidhamu haikuwa kitu chenye kipaumbele kwake.Sitaki kumzungumiza Mbwana Ally Samata.Wengi wanasema kuhusu Samatta na kiwango chake kwenye soka. Alibaini anacho kipaji na jukumu lake imebaki kulinda kipaji chake na kuheshimu misingi ya soka. 

Naona kuna tofauti kubwa kati ya Hasheem Thabeet na Mbwana Samata. Tujifunze kwa Hasheem na kisha tutafakari safari ya Mbwana Samatta.Sote tunajivunia mafanikio ya Samatta. Tuiangalie safari yake kisha tuangalie tumesimama upande upi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...