Benki ya Exim imekamilisha mwaka 2019 kwa kishindo! Ikiwa ni benki ya tano kwa ukubwa wa mali nchini Tanzania, Benki ya Exim imefanikiwa kutwaa idadi kubwa ya tuzo za kiufanisi katika sekta ya benki kutoka taasisi na mashirika mbalimbali ya kimataifa.

Wakati benki hiyo ikifanikiwa kutwaa tuzo ya 'Benki ya Bora ya Uwekezaji' nchini Tanzania kwa mwaka wa nne mfululizo kupitia tuzo za Global Banking and Finance Awards, pia huko nchini Djibouti benki hiyo kupitia tawi lake Benki ya Exim Djibouti ilifanikiwa kutwaa tuzo ya "Benki Bora ya Mwaka" kwa miaka mitatu mfululizo huku pia tawi la benki hiyo nchini Comoros, Benki ya Exim Comoros ikitwaa tuzo ya ‘Benki Bora ya Ubunifu’ kwa mwaka 2019.

Akizungumzia tuzo hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bwana Jaffari Matundu alisema, "Benki ya Exim inafurahi kutambuliwa kupitia tuzo hizi muhimu katika mwaka uliopita wa 2019. Lengo letu ni kuendesha ukuaji wa bara la Afrika huku tukitoa huduma za kifedha zenye suluhisho sahihi. Utambuzi huu unaadhihirisha namna ambavyo tumejitoa kuwa zaidi ya watoa huduma za kifedha. Sisi ni kichocheo cha mabadiliko ya uchumi katika nchi zote ambazo tunaendesha huduma zetu kwa kufanya biashara sahihi kwa njia sahihi.” alisema.

"Suala la ubunifu ndio kipaumbele cha benki yetu na tuzo hizi ni ushahidi tosha wa namna tunavyojizatiti katika kutafuta njia bora za kutoa majawabu ya huduma za kifedha mataifa yote tunayotoa huduma zetu,’’

Bwana Matundu alihitimisha kwa kubainisha kuwa mbali na kuhisi ufahari, tuzo hizo zimeongeza chachu kwa benki hiyo iweze kwenda mbele zaidi huku akiwaahidi wateja wa benki hiyo watarajie huduma bora zaidi kutoka benki ya Exim.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...