Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
LICHA
ya kutajwa na jarida la Forbe kwa kuwa mwanamke tajiri zaidi barani
Afrika anayemiliki dola za kimarekani bilioni 2.2 (46) amekumbana na kashfa za ubadhilifu wa fedha kupitia mikataba kutoka
sekta ya ardhi, gesi, mafuta na madini wakati wa utawala wa baba yake
Jose Eduardo Did Santos aliyetawala kwa miaka 38.
Vyombo
vya habari nchini humo vimeripoti kuwa hati zilizovuja zinaonesha
utajiri huo umetokana na unyonyaji na ufisadi kutoka kwa nchi hiyo
ambayo ni tajiri zaidi katika maliasili.
Hati
hizo zinaonesha kuwa Isabela na mumewe waliruhusiwa kununua mali za
Serikali kupitia mikataba mibovu iliyopitishwa wakati wa uongozi wa baba
yake.
Isabela anayeishi
London, Uingereza na kumiliki mali nyingi huko yeye na mume wake ambaye
ni mfanyabiashara maarufu kutoka nchini Kongo na mama wa watoto wa tatu
amekana madai hayo na kueleza kuwa hizo ni vita vya kisiasa kwa Serikali
iliyopo dhidi yake.
Isabela
ambaye alitangaza kuwania kugombea urais nchini humo kwa kueleza kuwa
uongozi ni kuhudumu na atafanya awezavyo katika maisha yake katika
kuhudumu katika nafasi hiyo.
Hadi
sasa tajiri huyo yupo chini ya uangalizi wa Mamlaka ya kupambana na
rushwa huku mali zake zilizopo ndani ya nchi zikiwa zimeshikiliwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...