Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

 VIONGOZI tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi wanasubiri hukumu yao baada ya leo Januari 24,2020 kufunga kesi yao kwa upande wa ushahidi wa utetezi baada ya kuwaita mashahidi 15 kati ya 200 ambao awali walisema wangewaita.


Washtakiwa hao kupitia Wakili wao Peter Kibatala wamedai hawakusudii kuita shahidi mwingine kwani ushahidi uliotolewa na mashahidi waliofika mahakamani hapo unajitosheleza hivyo hawaoni haja ya kuita shahidi mwingine.

Hata hivyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewapa onyo kali Mbunge wa Kawe Halima Mdee na Mbunge wa  Bunda Ester Bulaya kutokana na kukiuka masharti ya dhamana zao kwa kutoka nje ya mipaka ya Tanzania bila kupata kibali cha Mahakama.

Akitoa uamuzi huo mahakamani hapo, Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amesema upande wa mashitaka umedhibitisha na hauna wasi wasi kuwa mshitakiwa Mdee na Bulaya walikiuka masharti ya dhamana zao kwa kusafiri nje ya nchi bila kibali.

Pia amesema,  barua ya daktari wa Aga Khan waliyowasilishwa mahakamani hapo na haina maana yoyote kwenye mkataba wao wa dhamana na kwamba mahakama inatoa onyo kali kwa washitakiwa wote tisa katika kesi hiyo.

"Sijaona ni vizuri kuwafutia dhamana washitakiwa hawa wala kuwaambia wadhamini walipe fungu la dhamana waliyosaini, mahakama inawaonya washitakiwa wote na pia haitashikiria hati zao za kusafiria," amesema

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 24, mwaka huu ambapo pande zote mbili zitawasilisha majumuisho yao ya mwisho kabla ya hukumu kutolewa.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...