Na Yassir Simba, Globu ya Jamii

Klabu ya Yanga imeendelea kupata vipigo mfululizo baada ya leo kupoteza tena dhidi ya wenyeji wao 1-0 katika dimba la taifa Azam Fc wanalambalamba

Bao la Azam Fc limepatikana dakika ya 25" baada ya beki wa Yanga kujifunga katika harakati za kuokoa mpira uliochezwa na golikipa Farouk Shikalo

Yanga ilipata pigo tena mnamo dakika ya 80" ya mchezo Ally Sonso alipata kadi ya pili ya njano na kuzaa kadi nyekundu iliyowafanya Yanga kubaki pungufu hadi  dakika 90 Azam 1 - Yanga 0.

Kikao baina Ya wachezaji wa Yanga na Viongozi wa klabu hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Dkt. Mshindo Msola kinaendelea katika vyumba vya kubadilishia nguo katika dimba la taifa kufuatia vipigo viwili mfululizo kwa timu hiyo.
Kocha wa Yanga SC Luc Eymael alipokuwa akitoa maelekezo wakati wa mchezo wake na timu ya Azam SC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...