KAMPUNI ya kuzalisha bidhaa za umeme wa jua Zola imeahidi  kuwazawadia mitambo ya Zola  wanafunzi wa kidato cha nne watakaofaulu vizuri mwaka huu ili iwe chachu kwao ya kujisomea zaidi.

Ahadi hiyo ilitolewa jana Jijini Arushawakati wa uzinduzi wa ofisi ya Zola mkoani Arusha,Mkurugenzi wa Kampuni ya Zola Afrika Mashariki Yusuph Nassor alisema serikali ya sasa imejilota mumsaidia mtoto kielimu kwa kutoa elimu bure, hivyo na wao wanaunga mkono jitihada hizo.

Licha ya kusaidia sekta ya elimu pia watajielekeza kutoa sehemu ya faida yao kwa kusaidia sekta ya afya na nyingine.

Naye Mkuu wa Wilaya Longido Frack Mwaisumbe akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alippngeza kampuni hiyi kwa kuamua kusaidia serikali katika sekta ya elimu.

"Kwa kutoa zawadi hizi kutachangia kuinua elimu na watoto watasoma kwa uahindani na kuinua mkoa wetu kielimu,"alisema.Mwaisumbe alisema  baada ya zawadi hizo kutolewa mkoa utafanya vizuri  kitaifa  zaidi ya mwaka jana 2019 iliposhika nafasi ya tatu katika matokeo ya kidato cha nne. 

Pia aliipongeza kwa kuajiri vijana wakitanzania wengi  na kuwa kampuni ya kwanza  yakizalendo.Balozi wa Kampuni ya Zola, Idris Sultan aliahidi kuitangaza zaidi kampuni hiyo ili watanzania hasa wa pembezoni wasio na fursa ya kutumia umeme wa Shirika la  Tanesco watumie wa Zola unaotegemea jua.

"Wengi hawajuwi umeme huu wa jua lakini nitatangaza kote niendako ili watu wauelewe na vijana pia nitawahamasisha  wanapojenga wawe na miundombinu ya Zola, kwani hata ukiwekewa wa Tanesco haizuii kutumia huu inakuwa faida kwako ukikatika wa Tanesco unawasha wa Zola, "alisema.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...