Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KIONGOZI wa kanisa la Inuka Uangaze, Nabii na Mtume Boniface Mwamposa ametangaza kusitisha makongamano ya kiibada kufuatia  vifo  vya watu 20 na majeruhi 16 vilivyotokea Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro siku ya Jumamosi, Februari mosi mwaka huu baada ya kukanyagana wakigombea kukanyaga mafuta ya upako yaliyowekwa katika milango ya kutokea  katika viwanja vya majengo mjini humo.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na kiongozi wa kanisa hilo wakati wa ibada iliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe kabla ya kuanza kwa ibada ya jumapili.

Mwamposa amesema kuwa kufuatia maafa hayo makongamano yote yamesitishwa kwa sasa na ratiba ya makongamano itatolewa hapo baadaye.

Kiongozi  huyo wa kanisa la Inuka Uangaze ameeleza kuwa;

“Kwa sasa makongamano mengi nimeyasimamisha kwa sababu ya jambo hili ambalo limetokea na tunaomba neema ya Mungu ikapate kusimama na watu na baada ya hapo ndipo nitaweka ratiba ya makongamano.” amesema Mwamposa.

Hata hivyo kiongozi huyo ameeleza kusitisha kongamano la kukanyaga mafuta lililotakiwa kufanyika leo hii;

“Leo Jumapili ilipaswa liwe kongamano kubwa la kukanyaga mafuta lakini kwa sababu ya shida iliyotokea, tumesimamisha yote kupata utulivu wa kuomba Mungu atupe neema ya kupanga mipango upya, nitaongea mengi kwenye ibada,” amesema Mwamposa.

Aidha amesema kuwa;

“ Linapotokea jambo kama hili kila mmoja atazungumza lake, na hatuwezi kuongea mengi kwa sababu vyombo vya ulinzi na usalama vinachunguza jambo hilo, kwa hiyo nikiongea sana nitavuruga na kuharibu uchunguzi unaoendelea" ameeleza.

 Vilevile amesema kuwa, lililotokea ni jaribu na ametoa pole kwa wale wote waliopoteza wapendwa wao na waliopatwa na majeraha na kueleza kuwa jambo hilo lilitokea akiwa akiwa ameshatoka Moshi  akiwahi Dar es Salaam kwa kongamono jingine limeumiza na kushtusha.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...