Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
KATIKA kuadhimisha siku ya Usalama wa Mtandao Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeanzisha kituo cha kimataifa cha kukabiliana na majanga ya kompyuta kijulikanacho kama Tanzania Computer Emergency Response Team(TZ-CERT).

Akizungumza na wanafunzi wa shule za Msingi, Sekondari na Vyuo Vikuu kwa kuwapa elimu juu wakati wa maadhimisho ya simu ya usalama wa matandao, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Mhandisi James Kilaba, amesema kuwa teknolojia ya Intaneti imeleta mapinduzi Makubwa katika sekta mbalimbali kwa kuboresha mifumo na kubadili mifumo ya utendaji kuwa ya Kieletroniki.

Amesema pamoja na manufaa yatokanayo matumizi mazuri ya mtandao, matumizi mabaya ya yanaweza kusababisha athari kuwa kwa watumiaji hata miundombinu ya kutoa huduma mtandaoni na matokeo yake yakawa ni kupoteza taarifa, pesa na hata ukosefu wa huduma.

Hata hivyo katika kukabiliana na madhara yatokanayo na mtandao wananchi wameaswa kuto kutoa taarifa binafsi kama vile, majina, tarehe ya kuzaliwa na sehemu anayotoka kwa kutumia mtandao ingawa taarifa hizo zinaweza kutumika kwenye matukio ya uhalifu.

"Mtu mwingine anaweza kufanya uhalifu kwa nia ovu kwa kuchukua taarifa hizo na kuzitumia kwa kufanya udanganyifu na kujifanya kuwa yeye". 

"Takwimu zinaonyesha vijana wengi wameingia kwenye hatari ya kiusalama wa mtandao kutokana na kushirikishana nywila 'Password' za akaunti zao, suala hili ni miongoni mwa matukio ya kiusalama wa mtandao yanayowakairi vijana wengi na yaliyoshamili sana katika miaka ya hivi karibuni."Amesema Mhandisi Kilaba.

Mhandisi Kilaba amesema kuwa walengwa katika siku ya usalama wa mtandao walengwa ni sisi sote, mzazi, mlezi, mtoto, kijana, mwalimu, mwelimishaji na mfanyakazi wa sekta yeyote ile ili kuhakikisha kila mmoja ahakikishe usalama katika anga la mtandao dhidi ya matukio yanayohatarisha kiusalama.

Hata hivyo kauli mbiu ya siku ya usalama wa mtandao amabyo hufanyika kila jumanne ya pili ya Februali kwa mwaka huu ni PAMOJA KWA MANDAO BORA.

"Napenda kusisitiza kuwa ulinzi na usalama wa mtandao ni jukumu shirikishi ambapo kila mdau wa mawasilianonanawajibika kutekeleza na kuhakikisha usalama katika anga la mawasiliano unakuwepo." Amesema Mhandisi, Kilaa.

Katika Kuadhimisha siku ya usalama wa Mtandao pia wametoa zawadi kwa wanafunzi wawili wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ambao waliibuka washindi katika shindano la usalama wa mtandao ambao ni Godwin Mpapalika na Karim Muya baada ya wanafunzi zaidi ya 1,000 kushiriki katika shindano hilo.

Kwa upande Afisa Tehama wa Mamlaka ya Mawasilino Tanzania(TCRA), Irene Kihwili amewaasa wanafunzi wa shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vikuu hapa nchini kutumia Vizuri mtandao ili uweze kuwasaidia katika maisha yao ya elimu na si vinginevyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Mhandisi James Kilaba, akitoa cheti cha Ushiriki kwa Mshindi wa Shindano la Mtandao, Godwin Mpapalika  leo jijini Dar es Salaam katika siku ya Usalama wa Mtandao iliyofanyika katika katika Ukimbi wa mikutano katika Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM). 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Mhandisi James Kilaba, akimpa zawadi zawadi ya Komputa Mpakato na cheti cha Ushiriki kwa Mshindi wa Shindano la Mtandao, Karim Muya  leo jijini Dar es Salaam katika siku ya Usalama wa Mtandao iliyofanyika katika katika Ukimbi wa mikutano katika Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).  Kushoto ni Mshindi wa Shindano la Mtandao, Godwin Mpapalika.

Afisa Tehama wa Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA), Irene Kihwili akizungumza katika maadhimisho ya siku ya usalama wa mtandao iliyofanyika  katika ukimbi wa mikutano  katika jengo la Maktaba ya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.

 Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...